Pata taarifa kuu
DRC-ICC-SIASA

Chama kikuu cha upinzani chatishia kuandamana DRC

Upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umetishia kuandamana kupinga uchaguzi wa Desemba 23 kufuatia hatua ya Tume huru ya Uchaguzi na Mahakama ya Katiba kuamua kuzuia wagombea kadhaa wa upinzani ikiwa ni pamoja na kiongozi wa zamani wa kivita Jean-Pierre Bemba kuwania katika uchaguzi ujao.

Kiongoi wa upinzani DRC, Jean-Pierre Bemba.
Kiongoi wa upinzani DRC, Jean-Pierre Bemba. REUTERS/Francois Lenoir
Matangazo ya kibiashara

Mapema wiki hii Mahakama ya Katiba ilithibitisha hatua ya Tume huru ya Uchaguzi kumzuia Jean- Pierre Bemba kuwania katika uchaguzi wa urais wa Desemba 23 na kusema kuwa hana vigezo vya kugombea nafasi ya urais kufuatia hukumu aliyopewa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kwa kosa la kuhonga mashahidi..

Jumanne wiki hii chama cha MLC kilitoa wito kwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu "kuweka mambo sawa" kuhusu sheria inayomhukumu Bemba kwa kosa la kuhonga mashahidi.

Chama cha MLC kinabaini kwamba sababu kuu iliyomuangusha Bw Bemba kuwania katika uchaguzi wa urais wa Desemba 23 ni hukumu hiyo ya ICC

Hii ni "tafsiri potofu za sheria ya ICC ili kumzuia Bw Bemba katika uchaguzi wa urais wa Desemba 23, 2018," katibu mkuu wa chama cha MLC Eve Bazaiba ameandika katika barua iliyowasilishwa kwa Bibi Fabienne Chassagneux, mwakilishi wa ICC nchini DRC.

Chama cha MLC cha Jean-Pierre Bemba kimetangaza kuwa kitatangaza baadaye tarehe rasmi ya maandamano hayo , kufuatia uamuzi wa mahakama ya katiba kuondoa jina la mgombea kwenye nafasi ya urais Jean-Pierre Bemba katika uchaguzi mkuu ujao nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.