Pata taarifa kuu
MALI-UN-USALAMA

Mlinda amani ajeruhiwa katika shambulio Menaka

Askari wa kikosi cha Umoja aw Mataifa nchini Mali amejeruhiwa katika shambulio dhidi ya kambi ya kikosi hicho huko Menaka, kaskazini mwa Mali, vyanzo vya usalama na utawala vimebaini.

Askari wa Mali mbele ya helikopta iliyombeba Waziri Mkuu wa Mali, Menaka, Mei 9, 2018.
Askari wa Mali mbele ya helikopta iliyombeba Waziri Mkuu wa Mali, Menaka, Mei 9, 2018. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi haya mapya yanakuja wakati Rais wa Mali, Ibrahim Boubacar Keïta, aliyechaguliwa tena Agosti 20, amewazwa leo Jumanne asubuhi mjini Bamako. Rais Keita atajikita hasa na kufufua makubaliano ya amani yaliyosainiwa mwaka 2015 na kundi la waasi wa zamani wa Tuareg. Utekelezaji wake umekuwa na matatizo makubwa na haukuzuia vurugu kuenea kutoka kaskazini mpaka katikati mwa nchi na nchi jirani, Burkina Faso na Niger.

"Magaidi walishambulia kambi ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko Ménaka (kaskazini) kwa bomu. Askari mmoja wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Mali amejeruhiwa na kuna baadhi ya vifaa ambavyo vimeharibika," chanzo cha usalama kimeliambia shirika la Habari la AFP. Nchi anakotoka askari hiyo haikutajwa.

Taarifa kuhusu shambulio hilo imethibitishwa na afisa wa serikali ya Menaka. "Majengo mawili yaliyojengewa Ujumbe wa umoja wa Mataifa yameharibikakufuatia shambulio hilo," chanzo hicho kimesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.