Pata taarifa kuu
MALI-USALAMA

Makundi ya waasi yakosoa ripoti ya Umoja wa Mataifa Mali

Ripoti iliyotolewa na kundi la wataalam kutoka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu mchakato wa amani kaskazini mwa Mali imeibua mvutano katika baadhi ya makundi ya waasi kaskazini mwa Mali.

Wapiganaji wa kundi la waasi Kidal, Mali, Julai 13, 2016.
Wapiganaji wa kundi la waasi Kidal, Mali, Julai 13, 2016. AFP/SOULEYMANE AG ANARA
Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Mataifa umetoa ripoti kali kuhusu ya hali ya usalama inayoendelea nchini Mali. Ripoti hiyo yenye kurasa 71 imetolewa Alhamisi hii, na RFI imepata kopi.

Ripoti ya wataalam wa Umoja wa Mataifa inayahusisha makundi yaliyotia saini makubaliano ya amani ya Algiers, nchini Algeria, katika mashambulizi ya kigaidi na katika visa mbalimbali vya uhalifu. Mambo ambayo, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, husababisha mdororo wa usalama kwa nchi hiyo.

Shutma za kundi la wataalam wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mali ni kubwa. Kuna masula ya mashambulizi ya kigaidi dhidi ya vikosi vya usalama vya Mali, biashara haramu ya wahamiaji, biashara haramu ya madawa ya kulevya na suala la kuajiri askari wa watoto. Orodha ya majina yaliyotajwa katika ripoti hii ndefu.

Hayo yanajiri wakati ambapo ripoti haijachapishwa rasmi, huku viongozi wa makundi ya waasi wakikataa kupokea tena simu zao wanapoitwa.

Hata hivyo baadhi ya makundi ya waasi yamekosoa ripoti hiyo na kusema kuwa ni uzushi mtupu kwa lengo la kuwapaka matope.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.