Pata taarifa kuu
DRC-UCHAGUZI-SIASA

Batumike aliyehukumiwa kuwabaka watoto kugombea katika uchaguzi DRC

Mvutano umeibuka nchini DRC, baada ya Tume ya Uchaguzi (CENI) kukubali kupokea fomu ya mwanamgambo aliyehukumiwa kifungo cha maisha na mahakama kwa kuwabaka wasichana wadogo. Hatua hiyo imesababisha hasira kwa mashirika ya kiraia nchini DRC dhidi ya Tume ya Uchaguzi.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi DRC, Corneille Nangaa.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi DRC, Corneille Nangaa. MONUSCO/Alain Wandimoyi
Matangazo ya kibiashara

"Kesi yake kidogo ilituchanganya. Marekebisho yanaendelea," Tume ya Uchaguzi imeliambia shirika la Habari la AFP.

Fomu za Frederick Batumike, mwenye umri wa 64, zilipokelewa na kukubaliwa na Tume ya Uchaguzi na anatarajia kugombea katika uchaguzi wa manispaa ya Kabare katika mkoa wa Kivu Kusini, mashariki mwa DRC, kulingana na orodha ya awali ya Julai 26 inayopatikana kwenye tovuti ya Tume Uchaguzi (CENI) .

Julai 26 Mahakama ya kijeshi katika kitengo chake cha Rufaa ilithibitisha kifungo cha maisha dhidi ya Frederick Batumike kwa kuwabaka wasichana arobaini wenye umri kuanzia miezi 18 hadi miaka 12 katika eneo la Bukavu kati ya mwaka 2013 na 2016.

Alipatikana na hatia katika kesi ya mwezi Desemba na mahakama ya kijeshi "kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu, ubakaji na mauaji,". Alishtakiwa kuwa katika kundi la wanamgambo wa "Jeshi la Yesu".

Upande wa utetezi na mashirika yasiyo ya kiserikali yalikaribisha uamuzi huo wa mahakama na ushindi wa kihistoria dhidi ya kutoadhibu uhalifu unaohusiana na udhalilishaji wa kingono katika maeneo ya migogoro.

Shirika la kiraia la Nouvelle dynamique de la societe civile, linasema "limepigwa na butwaa baada ya kuona jina la Frederic Batumike kwenye orodha ya mwisho ya wagombea katika uchaguzi wa wabunge wa mkoa."

"Kuweka wahalifu na kuwatenga raia vingine kutokana na sababu za kisiasa na maagizo kutoka kwa viongozi wa juu kunaondoa imani kidogo na uaminifu kwa Tume ya Uchaguzi (CENI),"shirika hilo limesema katika taarifa yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.