Marekani yakosoa kauli za viongozi wa DRC
Hatua za mwisho za mchakato wa uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zimezua wasiwasi kwa Marekani, Kanisa Katoliki na shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Human Right Wacht (HRW).
Imechapishwa:
"Tuna wasiwasi sana na uamuzi wa Tume ya Uchaguzi wa tarehe 24 Agosti kuwaondoa wagombea wengine wa upinzani katika uchaguzi wa urais kwa kile kinachoonekana kuwa ni sababu za kisiasa," Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Nikki Haley alisema mapem awiki hii.
Faili za wagombea urais sita kati ya 25, ikiwa ni pamoja na kiongozi wa zamani wa kivita Jean-Pierre Bemba, hazikupokelewa na Tume ya Uchaguzi (CENI). Sita hao wamewasilisha malalamiko yao kwa Mahakama ya Katiba.
Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa pia ameitaja kuwa ni "kero" kauli ya rais Joseph Kabila na Tume ya Uchaguzi (CENI) kukataa msaada wowote kutoka nje kwa ajili ya uchaguzi uliopangwa kufanyika Desemba 23.
Ambassador Nikki Haley on upcoming elections in the #DRC: “Choose free, fair, & credible elections on December 23. Choose a peaceful transition of power in January 2019. And, by doing so, choose a better future for generations of Congolese to come.” More: https://t.co/birEdebKY8 pic.twitter.com/qCIxFNujaQ
US Mission to the UN (@USUN) August 27, 2018
"Tunaheshimu DRC kama nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa, lakini hiyo inaweza kuchochea uhasama wakati serikali ya DRC inakataa misaada ambayo itasaidia kuandaa uchaguzi huru, wa haki na wa kuaminika," alisema Haley.
Alikua akizungumza katika mkutano wa kufuatilia mchakato wa uchaguzi mbele ya wanachama kadhaa wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ikiwa ni pamoja na Ufaransa.