Pata taarifa kuu
NAMIBIA-UJERUMANI-USHIRIKIANO

Mabaki ya miili ya watu kutoka jamii za Herero na Nama kurejeshwa Namibia

Ujerumani inatazamia Jumatano wiki hii kurejesha mabaki ya miili ya watu kutoka jamii za Herero na Nama waliouawa mwanzoni mwa karne ya 20, mnamo mwaka 1904.

Esther Utjiua Muinjangue, kiongozi wa shirika llinalotetea haki kwa jamii ya Herero nchini Namibia, na wajumbe wa serikali ya Namibia, Agosti 27, 2018.
Esther Utjiua Muinjangue, kiongozi wa shirika llinalotetea haki kwa jamii ya Herero nchini Namibia, na wajumbe wa serikali ya Namibia, Agosti 27, 2018. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Wanahistoria wanachukulia mauaji hayo yaliyotekelezwa na Ujerumani dhidi ya maelfu ya watu kutoka jamii za Herero na Nama nchini Namibia kama mauaji ya kwanza ya kimbari ya karne ya ishirini.

Januari 12, 1904, watu kutoka jamii ya Herero, waliopokonywa sehemu za kuishi na mifugo yao katika eneo la jangwani Kusini Magharibi mwa Afrika (Namibia kwa sasa), waliendesha harakati za kupinga utawala wa kikoloni wa Ujerumani kati ya mwaka 1884 na 1915), harakati ambazo ziliongozwa na Samuel Maharero, na kuua raia 123 kutoka Ujerumani.

Mwaka uliofuata jamii ya watu wachache ya Nama pia iliendesha harakati za kupinga utawala wa wakoloni.

- Mauaji ya kimbari -

Baada ya kuzuka machafuko hayo, majeshi ya Ujerumani yalijibu na kutumia nuvu kupita kiasi ambapo yaliua watu wengi katika vita vya Waterberg, mnamo mwezi Agosti 1904. Wakati huo watu 80,000 waliljaribu kukimbilia katika nchi jirani ya Botswana. Majeshi ya Ujerumani yaliwafuata katika maeneo ya jangwani ya Kalahari ya leo, ambapo watu 15,000 ndio pekee walionusurika. Mnamo mwezi Oktoba 1904, Kamanda wa kijeshi wa utawala wa kikoloni, Jenerali Lothar von Trotha, aliamuru kuangamiza watu kutoka jamii ya Herero, huku akitangaza kwamba "kwenye mipaka ya Ujerumani (utawala wa kikoloni), mtu yeyote kutoka jamii ya Herero, awe na silaha au la, awe na mifugo au la anatakiwa kuuawa".

Kwa ujumla, watu takribani 60,000 kutoka jamii ya Herero na 10,000 kutoka jamii ya Nama waliuawa kati ya mwaka 1904 na 1908 katika kile amcaho wanahistoria wanataja kuwa ni mauaji ya kwanza ya kimbari karne ya ishirini.

Watu kutoka jamii ya Heroro ni 7% nchini Namibia wakati ambapo mwanzoni mwa karne ya 20 walikua 40%.

Mifupa ya watu kutoka jamii ya Herero na Nama, ikiwa ni pamoja fuvu 300 zilitumwa Ujerumani kwa ajili ya majaribio ya kisayansi ili kuthibitisha ukatili wa Wazungu kwa watu Weusi.

Mnamo mwaka 2008, balozi wa Namibia huko Berlin aliomba fuvu kurejeshwa nchini Namibia.

Mnamo mwaka 2011, Ujerumani ilirejesha nchini Namibia fuvu 20 za wapiganaji kutoka jamii ya Herero na Nama, ambazo zilipokelewa kwa heshima na umati wa watu huko Windhoek.

Mashirika ya kiraia nchini Namibia yanaiomba Ujerumani kuomba radhi na kukubali makosa walioyafanya kwa Wanamibia. jambo ambaloUjerumani haijatekeleza mpaka sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.