Pata taarifa kuu
DRC-EBOLA-AFYA

Watu kadhaa wapona virusi vya Ebola Mangina, DRC

Idadi ya watu wanaofariki dunia kutokana na ugonjwa hatari wa Ebola mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inaendelea kuongezeka na kufikia sasa vifo vya watu 70. Idadi hii ilitolewa na mamlaka nchini DRC Jumamosi jioni Agosti 25.

Léandre Kasereka, mwenye umri wa miaka 52, muuguzi katika Kituo cha Afya cha Mangina aliweza kupona ugonjwa hatari wa Ebola.
Léandre Kasereka, mwenye umri wa miaka 52, muuguzi katika Kituo cha Afya cha Mangina aliweza kupona ugonjwa hatari wa Ebola. Photo: Florence Morice / RFI
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, kutokana na kazi ya wahudumu waliohamasishwa dhidi ya ugonjwa huu, watu 13 sasa wamepona. Miongoni mwao, Leandre Kasereka, mwenye umri wa miaka 52, muuguzi katika Kituo cha Afya cha Mangina, ambako kulitokea mlipuko wa Ebola hivi karibuni. Aliambukizwa ugonjwa huo mwezi Julai, wakati watu wengi walioshukiwa kuambukizwa virusi vya Ebola walipelekwa katika kituo chake cha afya bila hata hivyo kujua iwapo waliambukizwa virusi vya ugonjwa huo. Tarehe 19 Agosti, Bw Kasereka aliondoka Kituo cha Matibabu cha Ebola, kilichojengwa huko Mangina na Shirika la Madaktari wasio na Mipaka (MSF).

Akihojiwa na RFI kwa nini mara kwa mara hua akitabasamu, Leandre amesema ni kutokana na kuwa "amepona ugonjwa hatari wa Ebola".

Bw Kasereka amesema kwanza alianza kutibiwa kama mgonjwa wa malaria.

Hata hivyo, ilichukua muda kwa muuguzi huyu kuhudumiwa vizuri. Alianza kuumwa mwezi Julai, wakati ambapo ilikua bado haijafahamika kuwa ni ugonjwa hatari wa Ebola mashariki mwa DRC na kuanza kutibiwa kama mgonjwa wa malaria. Hali yake ilizidi kuwa mbaya. Wakati serikali ilitangaza kuwa kumetokea mlipuko wa Ebola mashariki mwa nchi, mapema mwezi Agosti, alianza kuwa na wasiwasi kwamba tayari ameambukizwa virusi vya Ebola.

"Sikufikiria kwamba nitarudi kuwa mtu kama nilivya sasa. Nilikuwa nikifikiria kifo tu kwa sababu hii ni mara ya kwanza ugonjwa huu kuikumba jamii yetu. Ndiyo maana nilikua nikifikiria kifo, "Bw Kasereka amesema.

Mbali na maumivu ya ugonjwa alikuwa na wasiwasi kuhusu familia yake, mkewe na watoto wake 8. "Nilikua na mawazo mengi sana kuhusu familia. Chakula ... kila kitu, hasa kuwatafutia watoto chakula, mama watoto ndio alikua akihusika, "ameongeza.

Leandre Kasereka amewatolea wito wananchi wenzake kuharakia kwenye Kituo cha matibabu ya ugonjwa wa Ebola baada ya kuona dalili za ugonjwa huo ili kuepuka kuambukiza wengine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.