Pata taarifa kuu
DRC-EBOLA-AFYA

Ebola yaripotiwa katika maeneo ya waasi mashariki mwa DRC

Ugonjwa hatari wa Ebola unaoendelea kuiathiri Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo unaripotiwa katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi, mashariki mwa nchi hiyo. Watu wengi katika maeneo hayo wana wasiwasi kufuatia hali hiyo, Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza.

Maafisa wa afya wakibeba mwili wa mgonjwa wa Ebola ambao hajathibitishwa huko Mangina, karibu na Beni, mkoa wa Kivu Kaskazini, Agosti 22, 2018.
Maafisa wa afya wakibeba mwili wa mgonjwa wa Ebola ambao hajathibitishwa huko Mangina, karibu na Beni, mkoa wa Kivu Kaskazini, Agosti 22, 2018. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Kesi ya mtu aliyoambukizwa virusi vya Ebola iliyothibitishwa na kesi nyingine moja ya mtu anayedhaniwa kuambukizwa ugonjwa huo zimeorodheshwa katika mji wa kaskazini wa Oicha, katika mkoa wa Kivu Kaskazini, amesema Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani anayehusika na masuala ya majibu ya dharura, Peter Salama katika mkutano na waandishi wa habari huko Geneva.

Oicha haijadhibitiwa na waasi lakini eneo linalozunguka mji wa Oicha liko chini ya udhibiti wa waasi wa Uganda wa Allied Democratic Forces (ADF), kundi linaloshtumiwa kuhusika katika mauaji ya mamia ya raia tangu mwaka 2014.

"Kwa mara ya kwanza, tuna kesi ya mtu aliyeambukizwa virusi vya Ebola iliyothibitishwa (...) katika eneo lenye usalama mdogo," amesema Bw Salama.

"Hili ni tataizo ambalo tulifikiria mara kwa mara, na sasa tumeanza kuwa na wasiwasi ya hali hii," ameongeza.

Mlipuko wa ugonjwa wa Ebola kwa mara ya kumi nchini DRC uliripotiwa tarehe 1 Agosti huko Mangina,katika mkoa wa Kivu Kaskazini na kusababisha hadi kufikia sasa vifo vya watu 63 (kati ya watu 103 ambao wamethibitishwa au wameshukiwa kuwa na virusi vya Ebola), kwa mujibu wa afisa huyo wa WHO.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.