sikiliza tena
Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Matukio tuliyoyapa uzito wiki hii duniani
Rais wa DRC Felix Tshisekedi
 
Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/05 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/05 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/05 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Makundi ya waasi yawasilisha madai yao kwa Umoja wa Afrika CAR

media Askari wa Jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati waingia katika shule ya Koudoukou katika wilaya ya PK5, Bangui, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Desemba 13, 2015. © AFP

Makundi ya watu wenye silaha nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati yamewasilisha madai karibu mia moja, ikiwa ni pamoja na msamaha wa jumla, kwa kundi la wataalam wa Umoja wa Afrika (AU) ambalo linaendesha upatanishi na serikali ya nchi hiyo.

Kugawana madaraka na serikali ya umoja wa kitaifa, ujenzi wa barabara, msamaha wa jumla na uundwaji wa jeshi jipya: jopo la wataalam wa Umoja wa Afrika (AU) limeorodhesha madai 97 ya makundi ya watu wenye silaha nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa kurudi kwa amani.

Kwa mujibu wa mwanadiplomasia huko Bangui, wajumbe kutoka kila kundi la waasi wanatarajia kukutana na jopo la la wataalam wa Umoja wa Afrika huko Bouar, Magharibi mwa nchini, tarehe 27 Agosti ili kuweka mambo katika "usawa" kuhusu madai hayo, kabla ya kuyawasilisha kwa serikali kwa ajili ya makubaliano.

Msamaha wa jumla kwa wapiganaji wa makundi ya watu wenye silaha na viongozi wao ni miongoni mwa madai hayo. Hatua tata ambayo imekua ikiombwa na makundi hayo tangu kuanza kwa machafuko mnamo mwaka 2012.

Lakini serikali, ikiungwa mkono na jumuiya ya kimataifa, wamekua wakikataa madai hayo kama sharti la kusitisha uhasama. Mahakama Maalum ya Jinai (SPC) iliundwa ili kuhukumu uhalifu uliofanywa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati tangu mwaka 2003.

Madai mengine makubwa ni marekebisho ya mikataba ya ushirikiano wa kijeshi kati ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na Urusi. Tangu mwanzoni mwa mwaka 2018, Urusi imesaini makubaliano kadhaa ya aina hii na serikali ya Bangui, na kuibua hasira kwa baadhi ya makundi ya watu wenye silaha ambayo yanachukulia vibaya hatua ya Urusi kuitoa msaada wa silaha na vifaa vingine vya kijeshi kwa jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Jamhuri ya Afrika ya kati imeendelea kukabiliwa na mapigano ya hapa na pale kati ya makundi ya watu wenye silaha wanaopigania udhibiti wa maeneo na rasilimali za maeneo hayo. Serikali dhaifu ya nchi hiyo inadhibiti tu sehemu ya nchi.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana