sikiliza tena
Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Matukio tuliyoyapa uzito wiki hii duniani
Rais wa DRC Felix Tshisekedi
 
Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/05 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/05 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/05 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

DRC yajaribu kutokomeza ugonjwa hatari wa Ebola

media Maafisa wa DRC na wale wa Shirika la Afya Duniani (WHO) wamevaa nguo zinazowakinga na maambukizi ya virusi vya Ebola wakati mafunzo ya kukabiliana dhidi Ebola karibu na mji wa Beni, Kivu Kaskazini. REUTERS/Samuel Mambo/File Photo

Wizara ya afya nchini DRC imekubali, kutumiwa kwa dawa nyingine nne kuona iwapo inaweza kuwasaidia watu walioambukizwa ugonjwa hatari wa Ebola Mashariki mwa DRC.

Wiki iliyopita, maafisa wa afya walianza kutoa dawa inayofahamika kama mAb114 iliyotenegzwa nchini Marekani, kuona iwapo itawasaidia walioathiriwa.

Shirika la afya duniani WHO linasema watu 55 wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa huu tangu kuzuka mnamo mwezi Agosti katika mji mdogo wa Mangina, kilomita thelathini magharibi mwa mji wa Beni.

Ugonjwa huo ukiwa unaambukizwa kwa kupitia kumgusa mgonjwa na kwa njia nyinginezo, kuripuka kwake katika mji mdogo wa Mangina, pamoja na mji wa Beni, kumezusha wasiwasi miongoni mwa wakazi wa mji wa Beni.

Ugonjwa huo uliozuka siku chache tu baada ya serikali ya DRC kutangaza mwisho wa ugonjwa wa Ebola katika nchi hii.

Tatizo kubwa katika eneo hili ni kuwa, watu wanao uzoefu wa kula nyama za pori, bila ya kujuwa ikiwa nyama hizo zinazouzwa mitaani ni za wanyama waliouawa na wawindaji, au walifariki porini kwa magonjwa.

Kupigwa marufuku uwindaji, uuzaji na ulaji wa nyama toka mbuga za wanyama na taasisi inayohusika na kuhifadhi wanyama wa porini ICCN, kunaonekana kutoheshimiwa na wakazi, wanaowinda, kuuza na kula nyama za pori.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana