Pata taarifa kuu
MALI-UCHAGUZI-SIASA

Waangalizi wa kimataifa kutoa ripoti yao kuhusu uchaguzi Mali

Kiongozi wa Upinzani nchini Mali Soumaila Cisse amesema atatumia kila namna kudai ushindi wake ulioibwa katika duru ya pili ya uchaguzi uliofanyika nchini humo hivi karibuni, na kusema kwamba, kulikuweko na udanganyifu na wizi wa kura.

Cecile Kyenge, Mwangalizi Mkuu wa ujumbe wa waangalizi wa Umoja wa Ulaya, akihudhuria zoezi la uhesabuji kura huko Bamako, Mali Julai 29, 2018.
Cecile Kyenge, Mwangalizi Mkuu wa ujumbe wa waangalizi wa Umoja wa Ulaya, akihudhuria zoezi la uhesabuji kura huko Bamako, Mali Julai 29, 2018. REUTERS/Luc Gnago
Matangazo ya kibiashara

Haya yanajiri wakati waangalizi wa kimataifa waliopelekwa, wakitarajiwa kutoa ripoti yao kuhusu uchaguzi hio.

Duru ya kwanza ya uchaugzi wa Mali ilifanyika tarehe 29 Juni mwaka huu na kugubikwa na machafuko na mapigano makubwa ya silaha katika baadhi ya vituo vya kupigia kura.

Duru ya pili ya uchaguzi ilifanyika Agosti 12 ambapo rais anayemaliza muda wake alishinda kwa asilimia 67.17 ya kura dhidi ya mpinzani wake Soumaila Cisse ambaye alipata 32.83% ya kura.

Waziri huyo wa zamani wa fedha alijaribu wakati wa kampeni ya uchaguzi kukusanya sauti za upinzani. Soumaïla Cissé alishindwa kupata uungwaji mkono kutoka kwa Cheick Modibo Diarra na Aliou Diallo, ambao mmoja alichukua nafasi ya tatu na mwengine ya nne katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.