Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/04 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/04 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/04 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Wanafunzi zaidi ya 22 wapoteza maisha Sudan

media Wanafunzi wakihudhuria darasani chini ya kivuli cha mti katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Abu Shouk karibu na mji wa El Fasher, mji mkuu wa Darfur Kaskazini, Septemba 6, 2016. AFP

Wanafunzi 22 wamekufa maji baada ya boti lao kuzama Jumatao wiki hii kwenye mto Nile, katika mkoa ulio kwenye umbali wa karibu kilomita 750 kaskazini mwa mji wa Khartoum, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti.

Zaidi ya watoto 40 kwa jumla walikuwa wakisafiri na boti hilo.

Wanafunzi hao walikuwa wakienda shuleni wakati wa tukio hilo, kwa mujibu wa shirika la habari la Sudan Suna, ambalo pia limeripoti kifo cha mwanamke mmoja, na watu 23 waliojeruhiwa katika tukio hilo.

Ajali kama hizi zimekua zikitokea kwenye mto Nile nchini Sudan na kusababisha raia kuwa na wasiwasi wa kusafiri kupitia mto huo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana