Pata taarifa kuu
SUDAN-SIASA-USALAMA

Upinzani wapinga Al-Bashir kuwania katika uchaguzi wa mwaka 2020 Sudan

Nchini Sudan, upinzani umekataa uteuzi wa rais Omar al-Bashir kama mgombea wa chama chake katika uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika mwaka wa 2020.

Akiwania muhula wa tatukatika uchaguzi wa urais wa mwaka 2020, Omar al-Bashir atakuwa amekwenda kinyume na Katiba ya Sudan.
Akiwania muhula wa tatukatika uchaguzi wa urais wa mwaka 2020, Omar al-Bashir atakuwa amekwenda kinyume na Katiba ya Sudan. AFP PHOTO / ASHRAF SHAZLY
Matangazo ya kibiashara

Wiki iliyopita, Chama cha Omar Al-Bashir kilitangaza kuwa "kitachukua hatua muhimu za kuruhusu rais wa Sudan kuwania tena katika uchaguzi ujao". Hatua ambayo inapingana na Katiba ya mwaka 2005 ambayo inatia ukomo kwa uongozi wa rais kwa mihula miwili.

Omar al-Bashir, mwenye umri wa miaka 74, anatawala Sudan kwa karibu miaka 30. Aliingia madarakani mnamo mwaka 1989 kupitia mapinduzi ya kijeshi. Tangu kuanza kutumika kwa Katiba ya sasa mnano mwaka 2005, uchaguzi wa urais tayari umefanyika mara mbili mwaka 2010 na 2015, chaguzi ambazo zilisusiwa na upinzani.

Kulingana na katiba hii, ambayo inatia ukomo kwa uongozi wa rais kwa mihula miwili mbili, rais wa Sudan anapaswa kujiondoa katika kinyang'anyiro cha urais cha mwaka wa 2020. Hata hivyo, tamko la hivi karibuni la chama tawala linaibua maswali mengi kuhusu uwezekano wa marekebisho katiba, ambayo ni sheria mama nchini Sudan.

Sadek al-Mahdi, kiongozi wa upinzani wa kihistoria wa chama cha Ummah, amepinga mpango huo, huku akiaomba kuanzishwa kwa mpango wa kitaifa wa kukabiliana na hali hiyo. Kwa upande wake, chama cha RNM, cha Ghazi Salah al-Din, amesema katika taarifa kwamba wanataka kupambana dhidi ya uteuzi huu kwa kutumia "zana zote za kisiasa zilizopo."

Kwa upande wa waasi wa "haki na usawa" wanaopigana na serikali katika mkoa wa Darfur, wametaja kuwa mpango huo ni mauaji ya kikatiba unaotaka kutekelzwa na serikali isiyo rasmi. Itakumbuka kwamba Omar Al-Bashir anatafutwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa kivita, ICC, kwa uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya ubinadamu na mauaji ya kimbari katika vita vya Darfur.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.