Pata taarifa kuu
MALI-AFRIKA-SIASA

Raia wa Mali wapiga kura, katika duru ya pili ya uchaguzi

Raia wa Mali wanapiga katika duru ya pili kumchagua rais, katika Uchaguzi ambao umetishiwa na matukio ya kigaidi.

Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta akipiga kura Mjini Bamako hii leo
Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta akipiga kura Mjini Bamako hii leo REUTERS/Luc Gnago
Matangazo ya kibiashara

Wapiga kura nchini Mali, wanampigia kura rais wa sasa Ibrahim Boubacar Keita au mgombea wa upinzani Soumaila Cisse.

Duru ya kwanza ya Uchaguzi huu ulifanyika mwezi uliopita na kukosekana kwa mshindi aliyepata asilimia 50 ya kura.

Rais Keita baada ya kupiga kura leo asubuhi jijini Bamako, aliesema ana uhakika wa kuibuka mshindi, huku Cisse akisema ana matumaini ya kuibuka mshindi lakini anahofia wizi wa kura.

Cisse amekwenda katika Uchaguzi huu wa marudiano bila ya kufanikiwa kuwaunganisha wanasiasa wengine wa upinzani kumuunga mkono katika uchaguzi huu, suala ambalo wachambuzi wanasema huenda likamsaidia rais Keita kushinda.

Mshindi wa Uchaguzi huu, anasubiriwa na kibarua kigumu cha kupambana na utovu wa usalama hasa Kaskazini mwa nchi hiyo kutoka kwa makundi ya kijihadi.

Kuelekea Uchaguzi huu, magaidi walikuwa wametishia kutekeleza mashambulizi jijini Bamako.-

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.