Pata taarifa kuu
SUDAN-SIASA-USALAMA

Omar al-Bashir kuwania katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2020 Sudan

Chama tawala nchini Sudan kimemteua rais wa sasa wa nchi hiyo Omar al-Bashir kupeperusha bendera yake katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2020 kwa muhula wa tatu, kwa mujibu wa shirika la habari la serikali, Suna.

Rais wa Sudan Omar al-Bashir wakati wa hotuba yake kwa chama cha National Congress Party, Oktoba 23, 2014.
Rais wa Sudan Omar al-Bashir wakati wa hotuba yake kwa chama cha National Congress Party, Oktoba 23, 2014. REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah
Matangazo ya kibiashara

araza la Ushauri (Shura) la chama cha National Congress Party limefanya uteuzi huu baada ya mkutano usiku wa Alhamisi hadi Ijumaa mjini Khartoum, kwa mujibu wa Suna.

Hata hivyo Katiba ya Sudan pamoja na mkataba wa chama tawala, vinaruhusu mihula miwili kwa uongozi wa nchi hiyo kama rais. Kwa hivyo, nakala hizi zitapaswa kurekebishwa ikiwa Bw Bashir aatawania kwa muhula wa tatu katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2020 mwenyewe kuwachaguliwa mkuu wa nchi hiyo.

"Tuliamua kuchukua hatua muhimu ili kumuwezesha kuwania katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2020," aliwaambia waandishi wa habari Kiongozi wa Baraza la Ushauri wa chama tawala, Koko Kabashor bila kutoa maelezo zaidi kuhusu hatua hizo.

Bashir alichukua madaraka mnamo mwaka 1989 baada ya kumng'oa madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi Sadek al-Mahdi, waziri wa kwanza wa mwisho wa Sudan aliyechaguliwa chini ya misingi ya kidemokrasia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.