Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/11 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/11 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/11 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Mgombea urais kutoka kambi ya Kabila kutangazwa Jumatano hii

media Rais wa DRC Joseph Kabila, wakati wa mkutano na waandishi wa habari,Januari 26, 2018, huko Kinshasa. REUTERS/Kenny Katombe

Muungano wa vyama vinavyotawala nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo unatarajiwa kumtangaza mgombea wake wa urais leo Jumatano asubuhi.

Raia wengi wa nchi hiyo wanasuburi kuona ni nani atayepeperusha bendera ya muungano huo wakati huu rais Joseph Kabila ambaye kikatiba hastahili kuwania tena akiendelea kusalia kimya.

Ripoti kutoka jijini Kinshasa, zinasema kuwa viongozi wa muungano huo walikutana jana na kuamua kumweka wazi hivi leo mgombea wake, siku ambayo ndio ya mwisho kwa wanasiasa kurudisha fomu za kuwania urais kwa Tume ya Uchaguzi CENI.

"Washirika wote waliotia saini mkataba wa kuundwa kwa muungano wa vyama vinavyounga mkono serikali (FCC) walikutana Siku ya Alhamisi jioni katika mkutano muhimu huko Kingakati, " waziri ambaye hakutaja jina lake ameliambia shirika la habari la AFP.

“Sio siri tena, itakuwa suala la uteuzi wa mgombea ambaye atapeperusha bendera ya muungano wetu katika uchaguzi wa urais," ameongeza shirika mwingine wa karibu na rais Kabila ambaye pia hakutaja jina lake.

DRC ambayo ni moja ya nchi maskini zaidi Afrika licha ya rasilimali zake,haijawahi kushuhudia mchakato wa kupeana madaraka kwa amani tangu kupata uhuru kutoka mikononi mwa Ubelgiji Juni 30, 1960.

Tryphon Kin-Kiey Mulumba ambaye ni mshirika wa karibu wa rais Kabila aliwashangaza wengi baada ya kuomba nafasi ya kuwania urais.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana