Pata taarifa kuu
MALAWI-SIASA-DPP

Atupele muluzi kuwania urais nchini Malawi

Kiongozi wa Chama cha United Democratic Front Atupele Muluzi anatarajia kuwania urais katika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwaka nchini Malawi.

Atupele Muluzi, kiongozi wa Chama cha UDF nchini Malawi
Atupele Muluzi, kiongozi wa Chama cha UDF nchini Malawi Nyasa Times
Matangazo ya kibiashara

“Uchaguzi ni miezi tisa ijayo na tunapaswa kuandaa mikakati madhubuti na kuwaeleza raia wa Malawi mipango tulioyonayo kwa ajili ya kuiendeleza nchi yetu,”amesema Muluzi, ambaye kwa sasa ni waziri wa afya katika serikali ya Malawi.

Uchaguzi huo unaotajwa utakuwa na upinzani mkali, utafanyika kwa mujibu wa katiba ya Malawi inayotaka kufanyika uchaguzi kila baada ya miaka mitano.

Rais wa sasa Pater Mutharika ameshapitishwa na chama tawala cha Democratic Progressive Party, DPP kuwa mgombea, suala lililopelekea mvutano katika chama na kupelekea makamu wa rais Saulos Chilima kujiuzulu na kuanzisha vuguvugu jipya.

Chama kingine ni Malawi Congress Party, MCP ambacho kimepanga kumsimamisha Dr. Lazarous Chakwera.

Tangu ilipopata uhuru Malawi imetawaliwa na vyama vitatu ambavyo ni MCP kilichotawala kutoka mwaka 1964 hadi 1994, UDF kutoka mwaka 1994 hadi mwak 2006 na DPP ambacho kimekuwa madarakani tangu mwaka 2009.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.