Pata taarifa kuu
DRC-EBOLA-WHO

Watu 33 wafariki dunia baada ya kuambukizwa Ebola Mashariki mwa DRC

Wizara ya afya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inasema maambukizi mapya ya ugonjwa hatari wa Ebola umesababisha vifo vya watu 33, Mashariki mwa nchi hiyo.

Maafa mashariki mwa DRC kwa sababu ya Ebola
Maafa mashariki mwa DRC kwa sababu ya Ebola appsforpcdaily.com
Matangazo ya kibiashara

Mbali na vifo hivyo, Wizara hiyo inasema kuanzia tarehe 1 mwezi Agosti, maambukizi mapya  13 yameripotiwa katika jimbo la Kivu Kaskazini.

Hata hivyo, serikali ya DRC inasema inashirikina ana maafisa wa Shirika la afya duniani WHO kutoa elimu kwa wakaazi wa Mashariki mwa nchi hiyo ili kuepusha maambukizi mapya.

Maambukizi mapya ya Ebola, yaliripotiwa katika Wilaya ya Mangina, Kilomita 30 kutoka mjini Beni, wiki moja baada ya serikali ya DRC kutanagza kuwa hakukuwa na maambukizi mapya Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo.

Watalaam wa afya wametoa wito kwa wakaazi wa Mashariki mwa DRC, kudumisha usafi na kuepuka kugusana na watu wanaoshukiwa kuambukizwa ugonjwa huu hatari.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.