Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/03 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/03 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/03 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Polisi yazuia mkutano wa upinzani na waandishi wa habari Zimbabwe

media Siku moja baada ya makabiliano kati ya waandamanaji na polisi yaliyosababisha vifo kadhaa, polisi ya Zimbabwe imezingira makao makuu ya chama kikuu cha upinzani cha MDC, huko Harare Agosti 2, 2018. REUTERS/Mike Hutchings

Polisi ya Zimbabwe imezuia kufanyika mkutano wa upinzani na waandishi wa habari, mkutano ambao ungelifanywa na mgombea mkuu wa wapinzani na mgombea aliyeshindwa uchaguzi Nelson Chamisa.

Polisi wakiwa wamevalia mavazi yao maalumu yakuzuia mashambulizi ya mawe na vifaa vingine waliingia katika hoteli moja,ambapo kiongozi wa upinzani anglifanya mkutano na waandishi wa habari, na kuwalazimu waandishi wa habari kuondoka mara moja.

Wakati huo huo rais anayemaliza muda wake Emmerson Mnangagwa, ambaye ameshinda uchaguzi wa urais kwa 50.8 %, amewatolea wito raia wake kushikamana wakati huu wa mvutano wa kisiasa ukiendelea.

Hata hivyo upinzani umeendelea kutupilia mbali matokeo ya uchaguzi yaliyotolewa na Tume ya Uchaguzi (ZEC) na kuyataja kuwa ni ya uongo.

Umoja wa Mataifa umesema una wasiwasi mkubwa kutokana na matukio ya ghasia yaliyoibuka nchini Zimbambwe baada ya uchaguzi wa urais na kusababisha vifo vya raia.

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa watu watatu waliuawa kwenye mji mkuu Harare wakati wa vuta nikuvute iliyofuatia uchaguzi huo uliofanyika tarehe 30 mwezi uliopita.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia Naibu msemaji wake ametaka pande husika Zimbambwe zirejelee ahadi zao walizotoa katika tamko la ahadi ya uchaguzi na kanuni za mwenendo ili kuhakikisha mchakato wa uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu.

Ametoa wito kwa viongozi wa kisiasa na wananchi wa Zimbabwe wajizuie na kukataa aina yoyote ya ghasia wakati huu ambapo wanasubiri tangazo la matokeo rasmi ya uchaguzi huo.

Bwana Guterres pia ametoa wito kwa viongozi wa kisiasa na wagombea kwenye nafasi hiyo ya urais wasake suluhu zozote za tofauti zitakazojitokeza kwa njia ya amani, mashauriano na sheria.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana