Pata taarifa kuu
MALI-USALAMA-SIASA

Ibrahim Boubacar Keïta na Soumaïla Cissé kupambana dura ya pili ya uchaguzi

Nchini Mali, ni mara ya pili Ibrahim Boubacar Keita na Soumaïla Cissé wanapambana katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais. Wanasiasa hawa wawili wanafahamiana kwa muda mrefu na wanashiriki katika siasa kwa miaka mingi. Mambo mengi kuhusu wawili hawa yanafanana.

Rais anayemaliza muda wake nchini Mali Ibrahim Boubacar Keïta (kushoto) atapambana katika duru ya pili na kiongozi wa upinzani Soumaïla Cissé (kulia).
Rais anayemaliza muda wake nchini Mali Ibrahim Boubacar Keïta (kushoto) atapambana katika duru ya pili na kiongozi wa upinzani Soumaïla Cissé (kulia). STR, ISSOUF SANOGO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wawili hawa mmoja ni kutoka Kusini na mwengine kutoka Kaskazini

Ibrahim Boubacar Keïta anatoka katika mji wa Koutialia katika Jimbo la Sikasso, naye Soumaïla Cissé anatoka huko Niafunké katika Jimbo la Timbuktu. Walipokua bado wanafunzi, wanasiasa hawa wawili walikutana huko Dakar, nchini Senegal katika Chuo kikuu. Lakini wawaili hao walisoma katika vitngo tofauti.

Waliporudi nchini, wote walishiriki katika chama kimoja cha siasa: ADEMA, chama cha kihistoria cha Mali kilichoanzishwa baada ya utawala wa kiimla kuanguka nchini Mali. Chini ya utawala wa Alpha Oumar Konaré, walihudumu kama mawaziri katika serikali moja. Ibrahim Boubacar Keïta alikua Waziri wa Mambo ya Kigeni wakati ambapo Soumaïla Cissé alikua akishikilia Wizara ya Fedha.

Hata hivyo uchaguzi huu wa mwaka 2018 utakuwa kwao ni mara ya pili wanapambana katika uchaguzi wa urais. Mnamo mwaka 2013, Soumaïla Cissé alishindwa dhidi ya mshindani wake Ibrahim Boubacar Keita ambaye alipata zaidi ya 70%.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.