Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/03 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/03 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/03 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Rais wa Zimbabwe awataka wananchi kuwa watulivu

media Rais anayemaliza muda wake Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa. ZINYANGE AUNTONY / AFP

Rais Emmerson Mnangagwa amewatolea wito raia wake kuwa watulivu wakati ambapo jeshi limekuwa likiendelea kupiga doria katika mitaa mbalimbali ya mji wa mkuu Harare kwa kusubiri matokeo ya uchaguzi wa urais.

Kauli hiyo inakuja siku moja baada ya kuzuka mauaji yaliyosababishwa na ukandamizaji dhidi ya upinzani unaodai kuepo kwa njama za kuiba kura.

Kwa upande wake, Tume ya uchaguzi (ZEC) imewataka raia kuwa "wavumilivu", ikitangaza kuwa matokeo yatatolewa leo Alhamisi mchana au Ijumaa.

Wananchi wa Zimbabwe walishiriki uchaguzi Jumatatu wiki hii bila hata hivyo kushuhudiwa machafuko yoyote, ikiwa ni kwanza ya urais tangu Rais Robert Mugabe kutimuliwa madarakani mwezi Novemba baada ya miaka thelathini na saba katika madaraka.

Siku ya Jumatano, baada ya kutangazwa kuwa chama tawala cha Zanu-PF kimeshinda viti vingi kati bunge, hai iligeuka na kuwa machafuko, baada ya wafuasi wa upinzani kumiminika mitaani na kutawanywa na vikosi vya usalama na ulinzi. Chama cha Zanu-PF kiko madarakani tangu mwaka 1980.

Jeshi lilifyatulia risasi dhidi ya waandamanaji wa upinzani wakidai kuepo kwa njama za wizi wa kura. Watu watatu waliuawa, kwa mujibu wa polisi.

Mapema Alhamisi wiki hii, rais Mnangagwa ametoa wito wa kutatua mgogoro huo kwa "amanio" na upinzani, na kusema kuwa alikua katika mazungumzo na kiongozi wa upinzani, Nelson Chamisa, kujaribu "kutafutia suluhu" mgogoro huo.

Jumuiya ya kimataifa imekuwa na wasiwasi juu ya mvutano huo wa baada ya uchaguzi.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana