Pata taarifa kuu
DRC-BEMBA-SIASA-USALAMA

Wafuasi wa Jean Pierre Bemba wajiandaa kumpokea kiongozi wao

Makamu wa rais wa zamani na kiongozi wa upinzani nchini DRC Jean Pierre Bemba anatarajiwa kurejea nchini leo Jumatano Agosti 1, kama alivyoahidi katibu mkuu wa chama chake (MLC) Eve Bazaiba.

Makamu wa rais wa zamani DRC na kiongozi wa upinzani Jean-Pierre Bemba.
Makamu wa rais wa zamani DRC na kiongozi wa upinzani Jean-Pierre Bemba. REUTERS/Francois Lenoir
Matangazo ya kibiashara

Jean-Pierre Bemba aliteuliwa na chama chake kuwania katika uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika nchini DRC Desemba 23.

Hivi karibuni Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, ilimuachiliwa huru mnamo mwezi Juni baada ya kukata rufaa.

Chama cha MLC kimewatolea wito wananchi wa DRC, hususan wakaazi wa mji wa Kinshasa, kuja kumpokea kwa shangwe na vigelegele, kwa amani na furaha," Imesema taarifa hiyo iliyosainiwa na Katibu Mkuu Eve Bazaiba.

Kurudi kwa Bemba kunatarajiwa kusisimua upya na kutikisa siasa za Demokrasia ya Kongo, chama tawala tayari wametoa tamko kuwa Bemba hana vigezo vya kugombea nafasi ya urais nchini humo, kutokana na alikua mshitakiwa wa mahakama ya makosa ya jinai ICC.

Wafuasi wa Jean-Pierre Bemba wakikusanyika huko Gemena, RDC, Julai 30, 2018.
Wafuasi wa Jean-Pierre Bemba wakikusanyika huko Gemena, RDC, Julai 30, 2018. Junior D. KANNAH / AFP

Bemba, mwenye umri wa miaka 55, ambaye kwa sasa yuko nchini Ubelgiji, aliachiliwa huru kwa uamuzi wa majaji wa ICC mnamo mwezi Juni. Alihukumiwa mnamo mwaka 2016 hadi kifungo cha miaka 18 kwa mauaji yaliyofanywa na wanamgambo wake nchini Jamhururi ya Afrika ya Kati mapema mwaka 2000. Mapema mwezi Julai, mwendesha mashitaka wa ICC aliomba kuongezwa miaka mitano jela katika kesi nyingne inayohusiana na kuhonga mashahidi. Wanasheria wake walifutilia mbali mashiitaka hayo dhidi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.