Pata taarifa kuu
CAR-URUSI-USALAMA

Waandishi wa habari watatu wa Urusi wauawa Jamhuri ya Afrika ya Kati

Waandishi wa habari watatu kutoka Urusi waliuawa mapema wiki hii nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati na watu wasiojulikana ambao, kwa mujibu wa mamlaka za mitaa, waliendesha shambulio la kuvizia dhidi ya gari lao.

Henri Dépélé, Meya wa eneo la Sibut karibu kilomita 200 kaskazini mashariki mwa mji mkuu wa Bangui, amesema waandishi hao wa habari watatu waliuawa Jumatatu saa nne usiku na wapiganaji waliokua wamejificha katika msitu ulio kando ya barabara.
Henri Dépélé, Meya wa eneo la Sibut karibu kilomita 200 kaskazini mashariki mwa mji mkuu wa Bangui, amesema waandishi hao wa habari watatu waliuawa Jumatatu saa nne usiku na wapiganaji waliokua wamejificha katika msitu ulio kando ya barabara. REUTERS/Siegfried Modola
Matangazo ya kibiashara

Kituo kinachochapisaha habari mtandaoni nchini Urusi kimebaini katika habari kwenye ukurasa wake wa Facebook kwamba waandishi hao wa habari watatu walipelekwa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kuchunguza shughuli za kundi la Wagner, shirika la usalama la kibinafsi la Urusi ambalo linajulikana kwa kutuma askari mamluki kupigana nchini Ukraine na Syria kwa niaba ya serikali ya Urusi.

TsUR, shirika ambalo limechapisha uchunguzi mbalimbali juu ya rushwa katika familia ya Vladimir Putin, linafadhiliwa na Mikhail Khodorkovsky, aliyekuwa tajiri mkubwa wa mafuta ambaye amekuwa mmojawapo wa wapinzani wakubwa wa rais wa Urusi.

Vyombo kadhaa vya habari nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati na vile vya kimataifa viliripoti uwepo wa kundi la Wagner katika ardhi ya Jamhuri ya Afrika Kati tangu wakati Moscow ilipokabidhi silaha ndogo ndogo kwa idara za usalama za nchi hiyo na kupeleka mamia ya wakufunzi wa kijeshi na raia wa kawaida kutoa mafunzo kwa jeshi la nchi hiyo.

Henri Dépélé, Meya wa eneo la Sibut karibu kilomita 200 kaskazini mashariki mwa mji mkuu wa Bangui, amesema waandishi hao wa habari watatu waliuawa Jumatatu saa nne usiku na wapiganaji waliokua wamejificha katika msitu ulio kando ya barabara.

Msemaji wa ofisi ya rais nchini jamhuri ya Afrika ya Kati, Albert Yaloké Mokpémé, amesema miili ya wanahabari hao watatu iliokotwa karibu na Sibut na askariserikali.

Wizara ya Nje ya Urusi imethibitisha vifo vya wandishi hao wa habari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.