Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Mali: Msafara wa magari ya kijeshi washambuliwa Ségou

media Askari wa Mali, Julai 2018 huko Bamako. REUTERS/Luc Gnago

Ujumbe wa askari wanaotoa ulinzi kwa shughuli za uchaguzi nchini Mali ulishambuliwa Jumanne hii, Julai 31, katika Jimbo la Ségou. Askari wanne waliuawa katika shambulizi hilo la kuvizia. Hili ni shambulio la kwanza tangu kufanyika kwa uchaguzi wa urais wa siku ya Jumapili.

Askari wa Mali walikua wakitoa ulinzi kwa msafara wa magari ualiyokua yamebeba vifaa na kadi za uchaguzi. Shambulizi hilo linalodaiwa kutekelezwa na wanamgambo wa KIislamu, lilitokea kwenye barabara inayotokea Nampala- kuelekea Dogofri katika Jimbo la Segou, kaskazini mwa mji wa Bamako.

Askari wanne wa Mali waliuawa katika shambulio hilo, na kwa mujibu wa jeshi la Mali, kwa upande wa washambuliaji, "magaidi nane walipoteza maisha". Magari mawili ya jeshi la Malili bado hayajapatikana na hakuna anayejua hatima ya askari waliokuwa katika magari haya mawili.

Hii ni mara ya kwanza tangu kufanyika kwa uchaguzi siku ya Jumapili wanamgambo wa Kiislamu kuendesha shambulizi dhidi ya msafara wa magari yanayosafirisha vifaa na kadi za uchaguzi nchini Mali. Siku ya uchaguzi, katika baadhi ya maeneo ya katikati na kaskazini mwa nchi, wanamgambo wa Kiislamu walizuia uchaguzi kufanyika.

Hayo yanajiri wakati ambapo kambi ya rais Ibrahim Boubacar Keita na ile ya mshindani wake mkuu Soumaila Cisse zinaendelea, kila upande wanadai kuwa wanaongoza katika uchaguzi huo ambapo kura zinaendelea kuhesabiwa.

Hata hivyo waangalizi wanasema huenda kusiwe na mshindi katika mzunguko wa kwanza kwa sababu ya ushindani mkubwa kati ya wagombea hao wawili.

Iwapo mshindi hatapata ushindi wa asilimia 50 ya kura zote, Uchaguzi wa duru ya pili utafanyika tarehe 12 mwezi Agosti.

Huu ni uchaguzi ambao umewavutia wagombea 24.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana