Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Rais Mnangagwa na Chamisa wasema wanaelekea kupata ushindi mkubwa

media Kura zinaendelea kuhesabiwa nchini Zimbabwe REUTERS/Mike Hutchings

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa na kiongozi mkuu wa upinzani Nelson Chamisa, wote wanadai kuwa wanaelekea kupata ushindi mkubwa katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika siku ya Jumatatu.

Mnangangwa amesema, chama chake cha ZANU-PF kinapata matokeo mazuri huku Chamisa akisema chama chake cha MDC kinaelekea kupata ushindi mkubwa.

Kauli hii inaonesha kuwa, matokeo ya mwisho, yatakayotangazwa na Tume ya Uchaguzi kufikia mwisho wa wiki hii, yatazua mzozo kati ya wanasiasa hao wawili kuhusu mshindi wa kweli.

Kuelekea katika Uchaguzi huo wa kihistoria ulioshuhudia zaidi ya asilimia 70 ya wapiga kura wakijitokeza, upinzani ulidai kulikuwa na njama za Tume ya Uchaguzi kumsaidia Mnangagwa kushinda uchaguzi huo.

“Taarifa tunazozipata kutoka kwa wawakilishi wetu, zinaonesha kuwa tunapata ushindi, lakini tunasubiri matokeo kwa mujibu wa Katiba,” amesema Mnangagwa mwenye umri wa miaka 75, kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Naye Chamisa mwenye umri wa miaka 40, amenukuliwa akisema wako tayari kuunda serikali mpya.

“Tunaelekea kupata ushindi mkubwa sana, tumefanya vizuri na tuko tayari kuunda serikali mpya,” amesema Chamisa kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Huu umekuwa ni Uchaguzi wa kwanza, kufanyika bila ya kuwepo kwa rais wa zamani Robert Mugabe ambaye aliondolewa madarakani mwaka 2017, baada ya kuwa madarakani tangu mwaka 1980.

Waangalizi wa kimataifa wamesema kwa mara ya kwanza, wapiga kura walijitokeza na kupiga kura bila vitisho au vurugu.

Wachambuzi wa siasa wanaona kuwa yeyote atakayeshinda, anatarajiwa kuleta mabadiliko nchini humo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana