Pata taarifa kuu
MALI-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Kura zinaendelea kuhesabiwa Mali, rais Keita asema anaelekea kushinda

Kura zinaendelea kuhesabiwa nchini Mali, baada ya Uchaguzi wa urais kufanyika Jumapili iliyopita katika taifa ambalo limeendelea kushuhudia changamoto za kiusalama.

Mkuu wa waangalizi wa Umoja wa Ulaya Cecile Kyenge akiangalia zoezi la kuhesabu kura jijini Bamako nchini Mali
Mkuu wa waangalizi wa Umoja wa Ulaya Cecile Kyenge akiangalia zoezi la kuhesabu kura jijini Bamako nchini Mali REUTERS/Luc Gnago
Matangazo ya kibiashara

Machafuko yalishuhudiwa Kaskazini na maeneo ya kati ya nchi hiyo, baada ya makundi yanayopinga serikali ya Bamako kuharibu na kuchoma vifaa vya kupigia kura.

Ibrahim Boubacar Keita ambaye anatafuta muhula wa pili, kupitia msemaji wake Mahamadou Camara amesema rais huyo anaelekea kupata ushindi.

“Yupo katika nafasi nzuri sana ya kupata muhula wa pili,” amesema Mahamadou Camara.

Hata hivyo, ushindani mkubwa unatoka kwa Soumaila Cisse, Waziri wa zamani wa Fedha ambaye mwaka 2013 aliibuka mshindi.

Hata hivyo waangalizi wanasema huenda kusiwe na mshindi katika mzunguko wa kwanza kwa sababu ya ushindani mkubwa kati ya wagombea hao wawili.

Iwapo mshindi hatapata ushindi wa asilimia 50 ya kura zote, Uchaguzi wa duru ya pili itafanyika tarehe 12 mwezi Agosti.

Ni uchaguzi ambao umewavutia wagombea 23.

Mshindi wa Uchaguzi huu anatarajiwa kuwa na kibarua kikubwa cha kuendelea kuhakikisha kuwa usalama unaendelea kuwepo nchini humo, hasa Kaskazini mwa nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.