Pata taarifa kuu
COMOROS-SIASA-KATIBA

Kura ya ndio yashinda mabadiliko ya Katiba Visiwani Comoros

Wapiga kura Visiwani Comoro wamepitisha kwa asilimia 92.74 mabadiliko ya Katiba baada ya kufanyika kwa kura ya maoni.

Rais wa Comoro  Azali Assoumani (Kulia) akisalimiana na wananchi mjini Moroni
Rais wa Comoro Azali Assoumani (Kulia) akisalimiana na wananchi mjini Moroni TONY KARUMBA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hii inamaanisha kuwa, rais Azali Assoumani atawania tena nafasi hiyo mwaka 2021.

Assoumani alichaguliwa kwa mara ya katika nafasi hiyo mwaka 2016.

Tume ya Uchaguzi imetangaza kuwa, kura ya ndio ilishinda kwa kupata kura 172,240 ambayo ni sawa na asilimia 92.74 huku kura ya Hapana ikipata kura 13,338 sawa na asilimia 7.26.

Mwenyekiti wa Tume hiyo Ahmed Mohamed amesema idadi ya watu walijitokeza kushiriki katika kura hiyo ya maoni ni asilimia 63.9.

Kura hiyo ya maoni ilisusiwa na upinzani, ambao licha ya kutoshiriki, umedai kuwa kulikuwa na wizi mkubwa wa kura.

Kabla ya kufanyiwa marekebisho, Katiba ya Comoro ilipigiwa kura mwaka 2001, ilimtaka rais kuongoza kwa muhula mmoja wa miaka mitano huku akitokea katika visiwa vitatu vidogo vya Kisiwa hicho.

Hata hivyo, marekebisho ya Katiba hii yameondoa kipengele hicho na sasa, rais anaweza kutoka katika eneo lolote la kisiwa hicho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.