Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-KATUMBI

Katumbi kurejea DRC wiki hii kuanza harakati za kuwania urais

Mwanasiasa wa upinzani nchini DRC Moise Katumbi amesema anaomba ruhusu ya kurudi nyumbani wiki hii, ili kuwania urais mwezi Desemba.

Mwanasiasa wa upinzani DRC, Moise Katumbi, ambaye yuko uhamishoni
Mwanasiasa wa upinzani DRC, Moise Katumbi, ambaye yuko uhamishoni Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Katumbi ambaye amekuwa akiishi nchini Ubelgiji, amesema kwa sasa yupo jijini Johannesburg Afrika Kusini na tayari ameliandikia barua Shirika la safari za angaa nchini humo kumruhusu atue na ndege yake binafsi.

Gavana huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 53, alikimbilia uhamishoni mwaka 2016 baada ya kutofautiana kisiasa na rais Joseph Kabila.

Hata hivyo, ripoti zinasema kuwa hata iwapo Katumbi atarejea nchini humo hataruhusiwa kuwania kwa sababu sheria za Uchaguzi zinamtaka anayetaka kuwa raia awe ndani ya nchi hiyo kwa angalau mwaka mmoja.

Mbali na Katumbi, Makamu wa rais wa zamani Jean Pirre Bemba anatarajiwa kurejea nyumbani siku ya Jumatano baada ya Mahakama ya Kimataifa ya ICC kumwachilia huru.

Bemba anatarajiwa pia kuomba nafasi ya kuwania urais.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.