Pata taarifa kuu
COMORO-SIASA-USALAMA

Kura ya maoni yakabiliwa na mvutano mkubwa wa kisiasa Comoro

Wananchi wa Comoro wanapiga kura ya maoni Jumatatu wiki hii kwa minajili ya kuifanyia mageuzi katiba ya nchi hiyo. Wawanchi wametakiwa kupiga kura kufanya mageuzi ya Katiba hususan kuhusu mfumo wa uongozi wa visiwa hivyo kutoka muhula mmoja wa miaka mitano hadi mihula miwili.

Kisiwa cha Anjouan, Comoro (picha ya kumbukumbu).
Kisiwa cha Anjouan, Comoro (picha ya kumbukumbu). CC BY-SA 3.0
Matangazo ya kibiashara

Mageuzi haya pia yanahusu kufutwa kwa Mahakama ya Katiba na nafasi za makamu wa rais.

"Je, unakubaliana na marekebisho ya rasimu ya Katiba? "Hili ni swali kwa wapiga kura wa visiwa vya Comoro ambapo watatakiwa kujibu " ndiyo "au" hapana" lakini wakitoa majibu yao kwa kupiga kura.

Kulinagana na rasimu ya Katiba hii mpya, azimio la Bunge linaloishinikiza serikali halitakubalika. Wabunge hawataweza kupinga uamuzi wowote wa serikali.

Kulingana pia na rasimu hii mpya ya Katiba Mahakama ya Katiba imefutwa na mamlaka yake yanashikiliwa na Mahakama Kuu, hali ambayo imezua mvutano mkubwa, huku muungano wa vyama vya upinzani vikitoa wito wa kususia kura hii ya maoni.

Ismailla Mohamed, msemaji wa rais Azali tayari ameonya: kama kura ya "ndiyo" itapita, rais Azali atawania katika uchaguzi wa utakaoitishwa mnamo mwaka 2019.

Kwa upande wa upinzani, wanasema ni pigo kwa demokrasia. Upinzani umebaini kwamba, kura hiyo ya maoni ni kinyume cha sheria. Hata kura ya "hapana" inaharibu mchakato.

Baadhi ya waangalizi wana wasiwasi kuhusu hali ya mvutano inayoendelea kushuhudiwa na kukumbusha kuwa Comoros ilipitia mgogoro mkubwa wa kujitenga hadi kufikia makubaliano ya Fomboni na kuanzishwa mnamo mwaka 2001 utaratibu wa kuweka Katiba mpya. Katiba ambayo serikali inataka kufanyia mageuzi leo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.