Pata taarifa kuu
DRC-UFARANSA-UBELGIJI-USHIRIKIANO

Raia wa Ufaransa na Ubelgiji kunyimwa visa ya kuingia DRC

Serikali ya Kinshasa imezitaka balozi zake kutoa visa tu za kibinadamu au kwa sababu za afya kwa Wabelgiji na Wafaransa ambao wanataka kwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ikisema ni kulipiza kisasi kwa kufungwa kwa ubalozi wa Ulaya nchini humo, kwa mujibu wa ujumbe kutoka kwa Waziri mambo ya nje wa DRC.

Rais wa DRC Joseph Joseph Kabila.
Rais wa DRC Joseph Joseph Kabila. REUTERS/Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

"Ni dhahiri kwamba balozi za Ubelgiji na Ufaransa wanatoa tu visa za kibinadamu au kwa sababu za matibabu kwa wananchi wa DRC tangu kufungwa kwa Ofisi ya Schengen," ameandika Waziri wa Mambo ya Nje wa DRCi, Emmanuel Ilunga.

"Balozi zetu zote zimetakiwa kutekeleza masharti haya kwa kulipiza kisasi na kanuni ya usawa," Bw Ilunga ameongeza.

Ubalozi wa Ulaya unaosimamiwa na Ubelgiji, Ofisi ya Schengen, ulifungwa tangu mwanzoni mwa mwaka huu kwa ombi la serikali ya DRC. Ofisi hiyo ilikua ikishughulikia maombi ya visa kwa nchi 18 za Ulaya.

Kufungwa kwa ofisi ya Schengen ilikuwa moja ya hatua zilizotangazwa na serikali ya Kinshasa baada ya Ubelgiji kuikosoa wa serikali ya rais Kabila.

Hivi karibuni Ufaransa iliitolea wito serikali ya DRC "kufufua" mazungumzo na jumuiya ya kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.