Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Ajali ya ndege yaua watu watano DRC

media Askari wakitoa ulinzi karibu na ndege ndogo aina ya Antonov 32 iliyoanguka huko Goma, DRC Mei 26, 2008. © AFP

Watu watano wamepoteza maisha katika ajali ya ndege ndogo ya uchukuzi aina ya Antonov 2 ya shirika moja la ndege nchini humo. Ajali ambayo imetokea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia kwenye mpaka na Angola, kwa mujibu wa chanzo rasmi.

Ndege hiyo ya shirika la ndege la Air Kasai ilianguka baada ya kuondoka kutoka mji wa Kamako, kusini mwa DRC wakati ambapo ingeliunganisha safari yake hadi Tshikapa, kilomita zaidi ya 150 kaskazini mwa DRC.

"Ndege ilianguka katika msitu, kilomita 3 kutoka Kamako baada ya kuondoka kuelekea Tshikapa. Watu wawili pekee, rubani na abiria mmoja, ndio wamenusurika, lakini hawajaongea mapaka sasa. Tuna idadi ya watu watano ambao wamepoteza maisha katika ajali hiyo, "amesema naibu mkuu wa eneo hilo, Anacletus Muswa Kapinga Safia.

Mnamo mwezi Juni ndege ndogo ya iliyokua ilikodiwa na shirika la Chakula Duniani (WFP) ilipata ajali ilipokua akipaa angani huko Kamonia na kusababisha watu kadhaa kujeruhiwa.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana