Pata taarifa kuu
NIGERIA-USALAMA

Mgogoro kati ya wakulima na wafugaji watishia kuhatarisha usalama Nigeria

Mgogoro kati ya wakulima na wafugaji katikati mwa Nigeria umekwisha sababisha vifo vya watu wengi, mara sita zaidi ya Boko tangu mwanzoni mwa mwaka huu na unatishia "kuhatarisha usalama wa nchi," kulingana na ripoti ya shirika linalohusika na kutatua migogoro (ICG) iliyochapishwa Alhamisi wiki hii.

Nchini Mali, wafugaji kutoka jamii ya Fulani na mifugo yao.
Nchini Mali, wafugaji kutoka jamii ya Fulani na mifugo yao. RFI/David Baché
Matangazo ya kibiashara

Ushindani wa kupata ardhi na rasilimali, unatokana na kuwepo kwa watu wengi katika nchi hiyo yenye watu wengi barani Afrika, imekuwa "tishio kubwa zaidi la usalama," Inernational Crisis Group (ICG) imesema katika ripoti yake.

Watu wasiopungua 1,500 wameuawa katika machafuko kati ya wakulima, wengi wao Wakristo, na wafugaji, ambao wengi wao ni kutoka jamii ya watu wa kuhama hama na Waislamu tangu mwezi Septemba 2017, ripoti imebaini.

Kati ya idadi hiyo, zaidi ya watu 1,300 walipoteza maisha kati ya mwezi Januari na Juni, ikiwa ni mara sita zaidi kuliko idadi ya waathirika wa boko Haramu kaskazini mashariki mwa NIgeria.

ICG imetolea wito serikali kuongeza jitihada zake za kuzuia machafuko kabla ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwezi Februari mwaka ujao, machafuko ambayo husababisha mvutano wa kijamii, kidini na kisiasa.

Rais Muhammadu Buhari anashutumiwa kutowashukulia hatu wafugaji, Fulani kama yeye, ambao wamekua wakishtumiwa mara kwa mara katika vyombo vya habari vya Nigeria.

ICG inabaini kwamba hoja hii "haina nafasi", Buhari pia ameshindwa kuadhibu makundi ya watu wenye silaha ambayo wameendelea kuzorotesha usalama dhidi ya wafugaji kutoka jamii ya Fulani katika majimbo kadhaa ya kaskazini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.