Pata taarifa kuu
NIGERIA-USALAMA

Nane wauawa katika shambulizi la kujitoa muhanga dhidi ya msikiti Nigeria

Watu wanane wameuawa katika shambulizi la kujitoa muhanga lililoendeshwa leo Jumatatu asubuhi kwenye msikiti mmoja kaskazini mashariki mwa Nigeria , vyanzo vya kutoka eneo la shambulio vimesema.

Jimbo la Borno linaendelea kukumbwa na mashambulizi ya Boko Haram.
Jimbo la Borno linaendelea kukumbwa na mashambulizi ya Boko Haram. Bilyaminu/RFIHausa
Matangazo ya kibiashara

Mlipuko ulitokea katika wilaya ya Mainari Konduga katika jimbo la Borno, amesema Ibrahim Liman, mwanachama wa kundi la wanamgambo wa kiraia linalosaidia polisi katika mapambano yao dhidi ya wapiganaji wa Boko Haram, linaloendesha harakati zake katika eneo hilo.

"Mshambuliaji aliingia msikitini saa 5:15 Alfajiri wakati wa sala ya aAlfajiri na kujjilipua katika umati wa waumini waliokua katika sala. Watu nane walipoteza maisha papo hapo na watano walijeruhiwa," Ibrahim Liman ameliambia shirika la habari la AFP.

Umar Goni, mkaazi wa Konduga, aliiambia shirika la habari la AFP kwamba alikuwa njiani kuelekea msikitini wakati wa mlipuko na alishirikia katika zoezi la kusafirisha majeruhi hospitalini.

"Tutoa maiti saba katika vifusi na mtu mmoja aliyejeruhiwa , ambaye alifarwa mujibu wa mashahidi, mshambuliaji wa alikuwa na umri wa miaka ishirini.

Kundi la Boko Haram linaloongozwa na Abubakar Shekau, limekua kikiendesha mashambulizi dhidi ya raia wa kawaida, kwa mujibu wa serikali ya Nigeria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.