Pata taarifa kuu
SOMALIA-AL SHABAB-USALAMA

Al Shabab washambulia kambi ya jeshi Somalia

Wapiganaji wa Al Shabab waliokua wamejihami kwa silaha za kivita wameendesha shambulio dhidi ya kambi moja ya jeshi kusini mwa Somalia, na kuua watu kadhaa, kwa mujibu wa vyanzo vya kijeshi na mashahidi.

Uharibifu unaofanywa na Al Shabab, Somalia.
Uharibifu unaofanywa na Al Shabab, Somalia. REUTERS/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa vyanzo vya kijeshi katika eneo hilo, shambulizi hilo lililenga kambi ya kijeshi ya Bar-sanguni, kilomita 40 kaskazini mwa mji mkuu wa eneo hilo Kismayo.

Washambuliaji wa kujitoa muhanga walifaulu kuingiza gari lao lililokua limejaa vilipuzi kabla ya wapiganaji wa Boko Haram waliokua wamejihami kwa silaha za kivita kushambulia kambi ya kijeshi. Ufyatulianaji risasi ulidumu muda wa saa moja

"Al Shabab walishambuliwakambi ya kijeshi ya Bar-sanguni mapema leo asubuhi na mapigano yaikuwa makali.Vikosi vya ulinzi vya Somalia viliweza kuwarudisha nyuma wapiganaji wa Al Shabab lakini pande zote mbili zimepoteza wapiganaji," amesema Mohamed Bile, kamanda wa jeshi akihojiwa kwa simu kutoka kijiji jirani.

"Hatujakua na idadi kamili ya watu waliouawa katika shambulizi hilo, lakini huenda wakawa zaidi ya kumi," ameongeza.

Kundi la Al Shabab, lenye mafungamano na al-Qaida, limedai katika taarifa yake kuwa limeuawa askari 27 wa Somalia katika kambi hiyo "iliyojengwa na Marekani kwa wanamgambo waliopteza imani".

Al Shabab wanapiga kwa zaidi ya miaka kumi ili kuiangusha serikali ya Mogadishu, inayoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa.

Ingawa wamepoteza miji kadhaa na wilaya katika miaka ya hivi karibuni, kundi hili linaendelea kufanya mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya serikali, vikosi vya usalama au raia mjini Mogadishu na nje ya mji mkuu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.