Pata taarifa kuu
MAREKANI-SOMALIA-USALAMA-HAKI

Wakimbizi wa Somalia kupewa kibali cha kuendelea kuishi Marekani

Marekani imesema itawaruhusu raia wa Somalia 500 kusalia nchini humo kwa muda wa miezi 18 ijayo kwa sababu ya machafuko katika nchi yao.

Miili ya wakimbizi wa Somalia waliuawa katika mashambulizi katika pwani ya Yemen inatolewa kwenye boti iliyoegesha kwenye bandari ya Hodeida, mji unaodhibitiwa na waasi wa Houthi, Machi 17, 2017.
Miili ya wakimbizi wa Somalia waliuawa katika mashambulizi katika pwani ya Yemen inatolewa kwenye boti iliyoegesha kwenye bandari ya Hodeida, mji unaodhibitiwa na waasi wa Houthi, Machi 17, 2017. REUTERS/Abduljabbar Zeyad
Matangazo ya kibiashara

Hii inamaanisha kuwa, raia hao wa Somalia ambao walikuwa wanahofia kuondolewa kwa nguvu nchini humo, watapewa vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini Marekani hadi mwaka 2020.

Somalia ni baadhi ya mataifa ambayo serikali ya Trump imeiwekea vikwazo vya raia wa nchi hiyo ya Kislamu kuzuru Marekani kwa sababu za kiusalama.

Hivi kaibuni Marekani iliweka marufuku ya kusafiri kwa raia kutoka nchi sita zenye Waislamu wengi, ikiwa ni pamoja na Somalia, kwa kuhofia usalama wa taifa hilo.

Hatua hiyo ilikosolewa na nchi nyingi hasa nchi za Kiislamu kama vile Iran na Sudan.

Utawala wa Trump unasema watu wengi wanaoshukiwa kushirikiana na makundi ya kigaidi au makundi ya watu wenye msimamo mkali wa kidini wengi ni kutoka mataifa hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.