Pata taarifa kuu
DRC-KABILA-SIASA-USALAMA

Hotuba ya Joseph Kabila yasubiriwa na wengi DRC

Bunge na Seneti nchni DRC vimeitishwa katika kikao Alhamisi wiki hii ili kufuata ujumbe rais Joseph Kabila atakapokua akilihutubia taifa, siku sita kabla ya wagombea urais kuwasilisha barua zao za kuwania katika uchaguzi Mkuu ujao.

Rais wa DRC Joseph Kabila, Februari 14, 2018 huko Kinshasa.
Rais wa DRC Joseph Kabila, Februari 14, 2018 huko Kinshasa. REUTERS/Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

Rais Kabila hawezi kuwania kwenye kiti cha urais katika uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Desemba 23, kulingana na uamuzi wa taasi hizi mbili za bunge.

"Bunge na Baraza la Seneti vimeitishwa kwenye kikao Alhamisi hii Julai 19, 2018, saa tisa kamili," rais wa baraza la Seneti na Spika wa Bunge wameandika katika taarifa ya pamoja.

"Mada ni moja tu, yaani hotuba ya rais wa Jamhuri hali ya nchi," taarifa hiyo imebaini.

Wiki moja iliyopita, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, alisema kuwa rais Kabila anatarajia kutangaza mfululizo wa "maamuzi muhimu".

Bw Kabila amekuwa madarakani tangu mwaka 2001, muhula wake wa pili na wa mwisho ulimalizika mnamo mwezi Desemba 2016, Katiba haimruhusu kuwania muhula mwengine.

Uchaguzi wa rais uliotakiwa kumchagua mrithi wake uliahirishwa hadi Desemba 23, 2018.

Upinzani, mashirika ya kiraia, Kanisa Katoliki wanamshumu Bw Kabila, ambaye amekaa kimya kuhusu hatima yake ya kisiasa, kwamba anataka kuendelea kusalia mamlakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.