Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA-SIASA

Ripoti ya GEC yaishtumu serikali ya DRC kwa machafuko Kasai

Kundi la utafiti kuhusu Congo GEC limechapisha ripoti kuhusu mzozo unaozihusisha pande mbalimbali katika jimbo la Kasai, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Mji wa Tshikapa, mji mkuu wa Kasai ya Kati ulikumbwa na machafuko yaliyokua yakiendelea huko Kasai.
Mji wa Tshikapa, mji mkuu wa Kasai ya Kati ulikumbwa na machafuko yaliyokua yakiendelea huko Kasai. Google Maps
Matangazo ya kibiashara

Ripoti hiyo inakuja siku 15 baada ya Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kupokea ripoti kuhusu mzozo wa Kasai uliozihusisha pande zote, serikali na wanamgambo wa kundi la Kamuina Nsapu.

Ripoti hizo mbili zinataofautiana kuhusu jukumu la kila upande katika machafuko yalioshuhudiwa jimboni Kasai.

Ripoti hiyo ya GEC inatuhumu jukumu la serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia yaCongo katika mzozo huo na kulaani ukandamizwaji uliofanywa na vikosi vya usalama.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa hakuna uhusiano wowote wa mzozo huo wa Kasai na mchakato wa uchaguzi unaoendelea nchini DRCongo, wakati ripoti ya GEC inasema mzozo huo umechangiwa na swala la Rais Joseph Kabila kuendelea kusalia madarakani.

Hayo yanajiri wakati ambapo wanaharakati wa kutetea haki za binadamu mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wamekosoa mbinu za kijeshi zinazotumika kukabiliana na makundi ya kigaidi yanayosababisha mauaji katika eneo la mashariki mwa DRC.

Omar Kavota mwenyekiti wa shirika la kiraia linalotetea haki za binadamu na ustawi wa demokrasia CEPADHO amesema kinacholeta ugumu katika mapambano dhidi ya waasi ni mbinu za kawaida ambazo zinatumika badala ya mbinu maalumu za kumaliza makundi ya kigaidi.

Mashirika ya kiraia yamesikitishwa na namna ambavyo waasi hao waliweza kuvuka umbali mrefu na kuteketeza kambi ya jeshi bila jeshi kubaini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.