Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/10 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/10 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/10 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Jean-Pierre Bemba atangazwa mgombea urais na chama chake

media Wafuasi wa Jean-Pierre Bemba wakifurika mitaani mjini Kinshasa baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, kufuta hukumuiliyokua ikimkabili kiongozi wao, Juni 8, 2018. JOHN WESSELS / AFP

Chama cha upinzani cha MLC kimemtangaza rasmi kiongozi wa chama hicho, Jean-Pierre Bemba, kuwa mgombea wa kiti cha urais katika uchaguzi wa Desemba 23 mwaka huu nchini humo.

Hatua hiyo imechukuliwa baaada ya Bw Bemba kuachiliwa huru na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, siku kadhaa zilizopita, baada ya kushikiliwa na mahakama hiyo kwa zaidi ya miaka 3 kwa shutma za uhalifu dhidi ya binadamu, baada ya kuhusishwa katika mauaji yaliyotekelezwa na wapiganaji wake nchini Afrika Kusini.

Tangazo hilo lilitolewa wakati chama hicho kilipokua kikifungua mkutano wake Alhamisi wiki hii jijini Kinshasa.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, katibu mkuu wa chama hicho Eve Bazaiba amevitaka vyama vya upinzani kuungana pamoja katika kuhakikisha vinashinda kwenye uchaguzi huo.

Mbali na maelfu ya wafuasi wa chama hicho waliohudhuria mkutano huo mkubwa ni pamoja na Felix Tshisekedi wa chama cha Upinzani cha UDPS, Emmanuel Shadary wa chama tawala cha PPRD pia Vital Kamerhe wa chama cha UNC, Miongoni mwa wengine.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana