Siku ya Jumatatu Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed na Rais wa Eritrea Isaias Afwerki walitia saini kwenye "tamko la pamoja la amani na urafiki" huko Asmara kuashiria mwisho wa vita vya miaka 20 kati ya nchi hizo mbili.
Serikali za Addis Ababa na Asmara wamekubaliana kufufua uhusiano wa kidiplomasia kwa kufungua balozi zao, kuanzisha upya safari za ndege kati ya nchi hizo mbili na kushirikiana ili kuendeleza bandari ya Eritrea.
"Kwa ufunguzi wa ukurasa mpya wa amani na urafiki kati ya nchi hizi mbili, tunatarajia kurejesha safari za ndege aina ya Boeing 787 kuelekea Asmara," amesema Tewolde GebreMariam, meneja mkuu wa kampuni ya Ethiopia Airlines.