Pata taarifa kuu
MADAGASCAR-MAANDAMANO-USALAMA

Madagascar yakabiliwa na maandamano makubwa

Wafanyakazi 400 wa serikali wameandamana katika mji mkuu wa Madagascar, Antananarivo wakiitikia wito wa chama cha wafanyakazi. Wafanyakazi hao kutoka wizara ya Posta, Kilimo, Utumishi wa Umma, Elimu ya Taifa wameandamana wakiomba kutafutiwa ufumbuzi kwa madai yao.

Wafanyakazi 400 wa serikali waliandamana Alhamisi, Julai 5, 2018 wakidai kuongezwa mishahara.
Wafanyakazi 400 wa serikali waliandamana Alhamisi, Julai 5, 2018 wakidai kuongezwa mishahara. Sarah Tétaud/RFI
Matangazo ya kibiashara

Wafanyakazi hao wanadai nyongeza ya mishahara na kuboreshwa kwa mazingira ya kazi.

Wafanyakazi hao wanasema ni miaka 58 hawatendiwi haki, wakati ambapo hali ya maisha inaendelea kuwa mbaya zaidi.

Wafanyakazi wa vyama vya wafanyakazi wengi walidhani kungelifanyika mabadiliko , baada ya Aprili 21. Lakini wameendelea kukata tamaa, amesema Randria Falitsialonina, kiongozi wa chama cha wakaguzi wa ajira.

Majadiliano yanaendelea kuteua wawakilishi watano wa muungano ambao watawasiliana moja kwa moja na Waziri Mkuu na hivyo kutokea kwa mgogoro wa kisiasa. Wakati huo huo, maandamano yanatarajiwa kuendelea Ijumaa wiki hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.