Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Bajeti ya shughuli za kulinda amani za UN yashuka 6%

media Shughuli ya kulind amani ya Umoja wa Mataifa nchini DRC. cfr.org

Hatimaye nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zimeweza kuelewana kuhusu shughuli za kulinda amani baada ya wiki kadhaa za mazungumzo. Jumla ya dola bilioni 6.689 zitatengwa kwa shughuli 13 duniani kote.

Mapendekezo haya yalitolewa na utawala wa Donald Trump. Marekani ilitoa pendekezo la kupunguza bajeti ya shughuli za kulinda amani , suala ambalo Marekani ilikua ikitoa kama sharti la kuendelea kutoa mchango wake katika shughuli hizo za Umoja wa Mataifa. Lakini kwenye Dola milioni 600 iliyopunguzwa, theluthi tatu ni kutokana na kufungwa kwa tume ya Umoja wa Mataifa nchini Haiti, uamuzi uliotarajiwa kwa muda mrefu.

Wanadiplomasia wanahakikisha kwamba kupunguka kwa bajeti ya shughuli za kulinda Amani ni hakikisho kuwa kuna maendeleo chanya katika shughuli za kulinda Amani duniani, lakini athari zitakua kubwa kwa tume tatu za Umoja wa Mataifa, ikiwa ni pamoja na MONUSCO nchini DR Congo ambayo itapoteza Dola milioni 92, UNAMID katika jimbo la Darfur ambayo itajikuta imepungukiwa na Dola milioni 60 pamoja na Sudan Kusini ambapo tume ya Umoja wa Mataifa nchini humo inatumia bajeti ilio chini ya Dola milioni 100.

Tume hizi mbili za Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini na katika jimbo la Darfur zitapungukiwa na idadi ya askari wake, licha ya kuwa hali ya usalama bado tete. Wanadiplomasia wanabaini kwamba hali hiyo haitaleta madhara kwenye shughuli za tume hizo za Umoja wa Mataifa, laikini wataalamu wanasema, hata hivyo, kwamba kutakuwa na chaguo la kufanya na kwamba tume hizo haziwezi kutekeleza majukumu yao kwa kikamilifu, wakati ambapo idadi ya askari itapunguzwa.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana