Pata taarifa kuu
MISRI-HAKI

Mahakama yabadilisha hukumu kwa watu 1,500 waliohusishwa na ugaidi Misri

Mahakama ya rufaa nchini Misri imebadilisha hukumu iliyowaorodhesha watu 1,500 kama magaidi. Miongoni mwa watu mashuhuru waliokuwa katika orodha hiyo ni rais wa zamani Mohamed Morsi aliyeondolewa madarakani mwaka 2013.

rais wa zamani Mohamed Morsi aliyeondolewa madarakani mwaka 2013 ni miongoni mwa watu waliohukumiwa kama magaidi Misri.
rais wa zamani Mohamed Morsi aliyeondolewa madarakani mwaka 2013 ni miongoni mwa watu waliohukumiwa kama magaidi Misri. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Mahakama hiyo imetaka Mahakama ya chini kusikiliza tena kesi hiyo.

Kwa ujumla wafuasi 1,200 wanaoshtakiwa katika mahakama ya mkoa wa Minya wanatuhumiwa kuhusika na mauaji, jaribio la kuwaua askari kadhaa wakati wa ghasia zilizoibuka mwezi Agosti 14 wakati ambapo polisi ilihusika kuua mamia ya wafuasi wa rais Morsi pale walipozivamia kambi mbili za wafuasi hao kwa lengo la kuwatawanya. Maelfu ya wanachama wa Udugu wa kiislamu waliokamatwa na viongozi wa juu wa kundi hilo akiwemo Morsi wanakabiliwa na kesi.

Na kama haitoshi serikali ililitangaza kundi hilo kuwa la kigaidi ingawa Udugu huo wa kiislamu unasema umejitolea kutekeleza harakati za amani.

Umoja wa Ulaya na Marekani wamekua wakipaaza sauti kuikosowa hatua hiyo ya Mahamaka ya Misri. Umoja wa Ulaya amekua ukiutolea mwito Utawala wa Misri kuwatetendea haki washtakiwa katika kesi hiyo. Itakumbukwa kwamba tangu serikali hiyo ilipoingia madarakani imewashtaki zaidi ya wafuasi 2000 wa kundi hilo la Udugu wa kiislamu, baada ya kupinduliwa mwezi Julai rais aliyeingia madarakani kidemokrasia Mohammed Morsi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.