Pata taarifa kuu
GABON-CAR-USALAMA

Gabon yaamua askari wake kuendelea kubaki Jamhuri ya Afrika ya Kati

Nchi ya Gabon imeamua askari wake 444 waendelea kubaki nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati ambako wanashiriki katika Ujumbe wa unaosimamia Amani wa Umoja wa Mataifa katika nchi hiyo inayokabiliwa na mgogoro kwa miaka mitano sasa, taarifa kutoka serikali ya Gabon imesema

Askari wa vikosi vya Minusca nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wakiwa katika moja ya operesheni dhidi ya makundi ya wapiganaji
Askari wa vikosi vya Minusca nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wakiwa katika moja ya operesheni dhidi ya makundi ya wapiganaji UN Photo/Nektarios Markogiannis
Matangazo ya kibiashara

"Kwa kuitikia maombi mengi na wito wa rais wa (Jamhuri ya Afrika ya Kati) Faustin-Archange Touadéra pamoja na Katibu Mkuu" wa Umoja wa Mataifa, " serikali imekubali askari wa Gabon waendelea kushiriki katika Minusca, "Ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati," imesema taarifa iliyotolewa Jumatano usiku wiki hii.

Serikali ya Gabon inafanya hivyo" kwa jinakuonyesha mshikamano wa nchi za kiafrika na uhusiano mzuri wa urafiki na raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati", nakla hiyo imeongeza.

Hata hivyo serikali inasema kuwa "inashiriki katika kuundaa upya jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati katika suala la mafunzo, kwa kuwahudumia maofisa wa jeshi hilo katika shule za jeshi la Gabon."

Alipokua ziarani mjini Libreville mnamo Juni 14, Rais Touadéra alimwomba mwenzake wa Gabon Ali Bongo Ondimba askari wake kuendelea kushirika katika Minusma.

"Nimekuja kumwambia ndugu yangu Ali kwamba bado tunahitaji kikosi hicho katika jitihada zetu za utulivu," Touadéra alisema wakati huo.

Mnamo Machi, kwa mujibu wa afisa wa Umoja wa Mataifa wakati huo, kufuata "matatizo ya vifaa na unyanyasaji wa kijinsia", Gabon iliamua kuwaondoa askari wake 444 katika Ujumne wa Umoja wa Matiafa (Minusca).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.