Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-MAPINDUZI-HAKI-USALAMA

Mtuhumiwa amhusisha Gilbert Dienderé katika jaribo la mapinduzi Burkina Faso

Katika siku yake ya nne ya kuwahoji watuhumiwa wa jaribio la mapinduzi la Septemba 2015 nchini Burkina Faso, kwa mara ya kwanza, afisa wa zamani wa kikosi cha ulinzi wa rais amemhusisha Jenerali Gilbert Diendéré katika jaribio hilo.

Jenerali Gilbert Diendéré, katika ikulu ya rais Ouagadougou, Septemba 17, 2015.
Jenerali Gilbert Diendéré, katika ikulu ya rais Ouagadougou, Septemba 17, 2015. AFP PHOTO / AHMED OUOBA
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Jean Florent Nion, mkuu wa zamani wa majeshi ya Blaise Compaoré, yeye ndiye alitoa amri ya kuipindua serikali. Afisa huyo wa zamani wa kikosi cha ulinzi wa rais kilichovamia kikao cha baraza la mawaziri ameelezea jinsi viongozi wa serikali walivyokamatwa.

Jean-Florent Nion hakuficha kile kilichoandaliwa katika jaribio hilo la mapinduzi. "Jenerali Gilbert Diendéré ndiye ambaye aliamuru kufanya mapinduzi" amerejelea kauli hiyo mara kadhaa mbele ya majaji.

"Mnamo Septemba 16, 2015, baada ya kuanza kikao cha baraza la mawaziri, nilikwenda kwenye chumba cha pili," amesema afisa huyo, huku akieleza kwamba maofisa wawili walikuja kumwambia kuwa "Jenerali Gilbert Diendéré ameamuru kufanya mapinduzi".

Ili kuhakikisha kwamba amri ilitoka hasa kwa mkuu wa zamani majeshi ya Blaise Compaoré, alijielekeza nyumbani kwake na aliporudi, alimwambia afisa Eloi Badiel maneno hayo: "mkuu ana taarifa ya hali hii".

"Nilikuwa katika nafasi isiyofaa wakati usiofaa"

Papo hapo, mtu aliyekuwa afisa wa idara ya usalama wa rais wa mpito Michel Kafando aliingia katika gari hadi ikulu. Mara tu baada ya kuingia katika chumba cha mikutano, afisa Moussa Nebié - almaarufu Rambo - inasemekana kuwa aliiambia mawaziri kwamba ofisi ya rais inalengwa na mashambulizi na kuamuru rais Michel Kafando na Waziri Mkuu Yacouba Isaac Zida kumfuata.

Afisa Jean Florent Nion amebaini kwamba kujua kinachotokea, kwa sababu alikuja kupata habari kwenye televisheni ya taifa aliposikia kuwa kumeundwa Baraza la Kitaifa kwa kulinda Demokrasia, taasisi ya kisiasa ya maafisa waliojaribu kufanya mapinduzi. "Nilikuwa katika nafasi isiyofaa wakati usiofaa, hivyo basi sikua na maamuzi mengine," amekiri Jean Florent Nion.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.