Pata taarifa kuu
SENEGAL-HAKI

Karim Wade azuiwa kuwania urais Senegal

Karim Wade mtoto wa rais wa zamani wa Senegal Abdulaye Wade amezuiwa kuwania urais katika uchaguzi ujao licha ya chama cha baba yake cha Senegal Democratic Party kilichonundwa na baba yake kupendekeza asimame kwa tiketi ya chama hicho.

Karim Wade (kulia), mwana wa rais wa zamani wa Senegal Abdoulaye Wade.
Karim Wade (kulia), mwana wa rais wa zamani wa Senegal Abdoulaye Wade. AFP PHOTO / GEORGES GOBET
Matangazo ya kibiashara

Ofisi kuu ya uchaguzi nchini Senegal imetupilia mbali kuorodheshwa kwa Karim Wade katika majina ya wagombea wa Urais nchini Senegal.

Bernard Cassimir Scisse mkurugenzi wa ofisi kuu ya uchaguzi amesema, sheria ya uchaguzi haimruhusu mtu aliewahi kuhukumiwa kifungo cha miaka 5 na zaidi kuwania nafasi ya uchaguzi.

Karim Wade kwa sasa anasiku 15 kukata rufaa iwapo nia yake ya kuwania nafasi ya Urais itabaki kuwa palepale na kuiwasilisha katika ofisi ndogo ya ubalozi wa Coweit ambako aliwasilisha ombi la kuwania urais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.