Pata taarifa kuu
AU-RUSHWA-UGAIDi-USALAMA

Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika wanakutana Mauritania

Mkutano wa siku mbili wa wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika, umeanza nchini Mauritania. Zaidi ya marais na viongozi wa serikali kutoka nchi 40 wanakutana katika mji mkuu wa Mauritania, Nouakchott.

Paul Kagame,hapa ilikua Juanuari 28, 2018 Addis Ababa, akichukuaurais wa  kupokezana wa Umoja wa  Afrika.
Paul Kagame,hapa ilikua Juanuari 28, 2018 Addis Ababa, akichukuaurais wa  kupokezana wa Umoja wa  Afrika. SIMON MAINA/AFP
Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao wamekutana kujadiliana kuhusu, hali ya usalama, namna ya kupambana na ufisadi lakini pia wanajadili wanavyoweza kupata fedha kufadhili miradi mbalimbali. Namna ya kufanya biashara bila vikwazo, barani Afrika ni suala ambalo pia linajadiliwa.

Kiongozi wa Rwanda Paul Kagame, ambaye anashikilia urais wa kupokezana wa Umoja wa Afrika ( AU )wenye wanachama 55, atatoa pendekezo la kuhimiza biashara huru.

Mwezi Machi , mataifa 44 yalitia saini mkataba kuunda eneo la biashara huru la bara la Afrika , African Continental Free Trade Area, (CFTA), unaoonekana kuwa ni eneo kubwa kabisa la kibiashara duniani kwa mujibu wa nchi zinazoshiriki.

Kwa hivi sasa, mataifa ya Afrika yanafanya baina yao biashara ya kiasi cha asilimia 16 tu , kiasi kidogo cha biashaa ya kimkoa ikilinganishwa na mataifa ya America kusini, Asia, Amerika kaskazini na Ulaya.

Vita dhidi ya rushwa

Kupambana dhidi ya rushwa ni lengo kuu la mkutano huo, wanaopambana na rushwa wataangalia kwa kina kile ambacho Afrika inalenga kufanya katika kupunguza sifa yake kuwa ni eneo lililochafuka zaidi katika kufanya biashara duniani.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anatarajiwa kukutana na viongozi hao Jumanne wiki hii, huku ikitarajiwa kuwa atatangaza uungwaji wa nchi yake katika kusaidia kupambana na ugaidi barani Afrika hasa katika eneo la Sahel.

Katika bajeti ya AU ya dola milioni 769, dola milioni 451 zinatoka kwa wafadhili wa kigeni, ambao huchangia pia asilimia 97 ya mipango yake.

Umoja wa Afrika (AU) ni muungano wa mataifa 54 ya Afrika. Lengo lake ni kuimarisha ushirikiano wa kisiasa na kiuchumi wa bara hilo.

AU ilianzishwa mwaka 2001 mjini Addis Ababa kuchukuwa nafasi ya Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU). Maamuzi muhimu kabisa ya AU yanafanywa na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Afrika ambao unawakutanisha wakuu wa mataifa na serikali za nchi wanachama unaofanyika mara mbili kwa mwaka. Kamisheni ya Umoja wa Afrika ina makao yake makuu Addis Ababa, Ethiopia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.