Rais wa Zimbabwe awashtumu wafuasi wa Grace Mugabe kuhusika na shambulizi
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amehusisha kundi la wafuasi wa chama tawala cha Zanu PF waliojitenga na ambao wanamuunga mkono mkewe Robert Mugabe na mlipuko wa Jumamosi, mwishoni mwa juma lililopita.
Imechapishwa:
Mlipuko huo, uliotokea wakati Emmerson Mnangagwa alipokua akiondoka kwenye uwanja alipokua akiendesha mkutano wa kampeni za uchaguzi baada ya kuwahutubia wafuasi wake, ulisababisha vifo vya watu wawili.
Rais, ambaye amemrithi mtangulizi wake Robert Mugabe mnamo mwezi Novemba baada ya kumtenga, amesema anashuku G40, kundi la wafuasi wa Zanu-PF wanaomuunga mkono Grace Mugabe, kwa mujibu wa BBC.
Hajamshtumu Grace Mugabe kushiriki katika shambulizi hilo na amesema anasubiri watu zaidi kukamatwa kufuatia shambulizi hilo.