Pata taarifa kuu
DRC-BEMBA-SIASA-USALAMA

DRC: Bemba yuko huru kuchukua pasipoti maalumu zinatumiwa na maafisa wa serikali

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kupitia waziri wa mambo ya nje imesema kwa sasa makamu wa zamani wa rais Jean-Pierre Bemba anaweza kurejea nchini.

Kiongozi wa chama cha upinzani cha MLC Jean-Pierre Bemba.
Kiongozi wa chama cha upinzani cha MLC Jean-Pierre Bemba. REUTERS/JERRY LAMPEN
Matangazo ya kibiashara

Kauli hii inakuja siku chache baada ya kiongozi huyo wa zamani wa waasi kuachiliwa huru na mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).

Jean-Pierre Bemba anaweza kuomba pasipoti maalumu wanazotumiwa maafisa wa serikali ili kuweza kurudi nchini, baada ya kuachiliwa na ICC, ameandika katika barua Waziri wa Mambo y Nje wa DRC ikiwa imezalia miezi sita kabla ya Uchaguzi Mkuu, uliopangwa kufanyika tarehe 23 Desemba mwaka huu.

"Napenda kushukuru ikiwa utamuaomba Mheshimiwa Seneta (Jean-Pierre Bemba) kumtuma afisa wake wa itifaki kwenda kuchukua fomu ya maombi ya pasipoti maalumu kkwenye ubalozi wetu huko Brussels," ameandika Leonard She Okanye.

Bw Okitundu alikuwa akijibu ombi la Rais wa Bunge la Seneti la DRC Leon Kengo Wa Dondo.

Makamu wa rais wa zamani na mgombea urais mwaka 2006, Bemba aliondoka DRC mwaka 2007 baada ya kuzuka mapigano kati ya wanamgambo wake na jeshi la Rais Joseph Kabila.

Awali Waziri wa mambo ya nje wa DRC alisema kuwa Bemba "anaaweza kurudi nyumbani ikiwa anataka".

Kwa mshangao mkubwa, Jean-Pierre Bemba aliachiliwa huru baada ya kukata rufaa dhidi ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu, uhalifu uliotekelezwa na wapiganaji wake nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati mapema miaka ya 2000. Alihukumiwa miaka 18 jela katika mahakama ya mwanzo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.