Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-MAUAJI-JESHI

Mlipuko Adis Ababa wasababisha kifo na majeruhi 154

Mtu mmoja ameuawa huku zaidi ya mia moja hamsini wakijeruhiwa baada ya mlipuko wa guruneti katika mkutano wa kwanza kufanywa na waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed,jijini Adis Ababa na kusababisha mshtuko miongoni mwa wananchi.

Taharuki ilikumba jiji la Adis Ababa baada ya mlipuko
Taharuki ilikumba jiji la Adis Ababa baada ya mlipuko Yona Tadese/AFP
Matangazo ya kibiashara

Waziri mkuu huyo alikuwa akimalizia hotuba yake mbele ya makumi kwa maelfu ya wakazi wa jiji la Adis Ababa ndipo mlipuko ulipotokea na kuzua mshtuko ambapo wafuasi walikimbia kuelekea jukwaa wakati waziri mkuu huyo akiondolewa haraka na wasaidizi,alieleza mwandishi wa AFP.

Katika hotuba yake waziri mkuu Abiy baadae alisema tukio hilo lilitekelezwa na kundi ambalo hakulitaja lililolenga kuhujumu mkutano wake.

Abiy amesema wasiopenda amani ndio wametekeleza tukio hilo na kusema kuwa hawatafanikiwa kama ambavyo hawakuwahi kufanikiwa.

Nae waziri wa afya nchini humo Amir Aman ameandika katika ukurasa wake wa Twita kuwa takribani watu 154 wamejeruhiwa na mmoja amefariki dunia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.