Pata taarifa kuu
GAMBIA-USALAMA

Gambia: Mkuu wa polisi ajiuzulu baada ya vifo vya watu 3 Faraba Banta

Mkuu wa polisi nchini Gambia amelazimika kujiuzulu baada ya matukio ya Faraba Banta, kusini mwa Banjul, ambapo watu watatu walipoteza maisha siku ya Jumatatu wiki hii wakati polisi ilifyatua risasi kwa waandamanaji.

Faraba Banta,  Gambie ambako kulitokea vurugu baada ya polisi kuwafyatulia risasi waandamanaji.
Faraba Banta, Gambie ambako kulitokea vurugu baada ya polisi kuwafyatulia risasi waandamanaji. GOOGLE MAPS
Matangazo ya kibiashara

Wakazi wa mji huo walikusanyika na kuandamana kupinga uchimbaji wa mchanga ambao umekua ukitishia mazingira yao na mashamba yao ya mchele. Shinikizo hilo limesababisha Mkuu wa polisi kujiuzulu kwenye nafasi yake.

Barua ya kujiuzulu ya Landing Kinteh ilikubaliwa na rais siku ya Alhamisi wiki hii. Mkuu wa polisi alikosolewa na upinzani baada ya vurugu ya Faraba Banta. Hata hivyo alisema hakuwaagiza polisi kuwafyatulia risasi waandamanaji.

Mkuu wa Polisi alikuwa akihudumu kwenye nafasi hiyo kwa mwaka mmoja sasa. Kwa kusubiri uteuzi mpya, naibu wake, Alhagie Mamour Jobe, atamrejelea kwenye nafasi hiyo.

Maafisa watano wa polisi waliokua eneo la tukio walikamatwa pia. Na tume ya uchunguzi itaundwa kwa amri ya rais. Tume hiyo ambayo itajumuisha wanaharakati wa haki za binadamu, wanasheria, na mwakilishi wa serikali na polisi, itapewa mwezi mmoja tu ili kuweka wazi mazingira ya vifo vya raia hao watatu wa Gambia.

Rais Adama Barrow anatarajia kuzuru lro Ijumaa mchana mji wa Faraba Banta ili kukutana na familia za waathirika. Na zoezi la uchumbaji wa mchanga limesimamishwa kwa muda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.